Micah 4
1Katika siku za mwisho 1 mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa 2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote; 1 utainuliwa juu ya vilima, 2 na watu wa mataifa watamiminika humo.
2Mataifa mengi yatakuja na kusema, 1 “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, 2 kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. 1 Atatufundisha njia zake, 2 ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” 1 Sheria itatoka Sayuni, 2 neno la Bwana litatoka Yerusalemu. 1
3Atahukumu kati ya mataifa mengi, 2 na ataamua migogoro ya mataifa 2 yenye nguvu na yaliyo mbali. 1 Watafua panga zao ziwe majembe, 2 na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. 1 Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, 2 wala hawatajifunza vita tena. 1
4Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake 2 na chini ya mtini wake, 1 wala hakuna mtu atakayewaogopesha, 2 kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema. 1
5Mataifa yote yanaweza kutembea 2 katika jina la miungu yao; 1 sisi tutatembea katika jina la Bwana 2 Mungu wetu milele na milele. 1 Mpango Wa Bwana
6“Katika siku hiyo,” asema Bwana, 1 “nitawakusanya walemavu; 2 nitawakusanya walio uhamishoni 2 na wale niliowahuzunisha. 1
7Nitawafanya walemavu kuwa mabaki, 2 wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu. 1 Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayuni 2 kuanzia siku hiyo na hata milele. 1
8Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi, 2 ee ngome ya Binti Sayuni, 1 milki ya awali itarudishwa kwako, 2 ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.” 1
9Kwa nini sasa unalia kwa nguvu: 2 kwani huna mfalme? 1 Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate 2 kama ya mwanamke 2 aliye na utungu wa kuzaa? 1
10Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni, 2 kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, 1 kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji 2 ukapige kambi uwanjani. 1 Utakwenda Babeli; 2 huko utaokolewa. 1 Huko Bwana atakukomboa 2 kutoka mikononi mwa adui zako. 1
11Lakini sasa mataifa mengi 2 yamekusanyika dhidi yako. 1 Wanasema, “Mwache anajisiwe, 2 macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!” 1
12Lakini hawayajui 2 mawazo ya Bwana; 1 hawauelewi mpango wake, 2 yeye awakusanyaye kama miganda 2 kwenye sakafu ya kupuria. 1
13“Inuka upure, ee Binti Sayuni, 2 kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; 1 nitakupa kwato za shaba 2 na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” 1 Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana, 2 utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.