Micah 3
1Kisha nikasema, 1 “Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo, 2 enyi watawala wa nyumba ya Israeli. 1 Je, hampaswi kujua hukumu, 2
2ninyi mnaochukia mema 2 na kupenda maovu; 1 ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi 2 na kuondoa nyama kwenye mifupa yao; 1
3ninyi mnaokula nyama ya watu wangu, 2 mnaowachuna ngozi 2 na kuvunja mifupa yao vipande vipande; 1 mnaowakatakata kama nyama 2 ya kuwekwa kwenye sufuria 1 na kama nyama 2 ya kuwekwa kwenye chungu?” 1
4Kisha watamlilia Bwana, 2 lakini hatawajibu. 1 Wakati huo atawaficha uso wake 2 kwa sababu ya uovu waliotenda.
5Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, 2 mtu akiwalisha, 2 wanatangaza ‘amani’; 1 kama hakufanya hivyo, 2 wanaandaa kupigana vita dhidi yake. 1
6Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono, 2 na giza, msiweze kubashiri. 1 Jua litawachwea manabii hao, 2 nao mchana utakuwa giza kwao. 1
7Waonaji wataaibika 2 na waaguzi watafedheheka. 1 Wote watafunika nyuso zao 2 kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.” 1
8Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu, 2 nimejazwa Roho wa Bwana, 2 haki na uweza, 1 kumtangazia Yakobo kosa lake, 2 na Israeli dhambi yake. 1
9Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, 2 enyi watawala wa nyumba ya Israeli, 1 mnaodharau haki 2 na kupotosha kila lililo sawa; 1
10mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu 2 na Yerusalemu kwa uovu. 1
11Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, 2 na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, 2 nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. 1 Hata hivyo wanamwegemea Bwana na kusema, 2 “Je, Bwana si yumo miongoni mwetu? 2 Hakuna maafa yatakayotupata.” 1
12Kwa hiyo kwa sababu yenu, 2 Sayuni italimwa kama shamba, 1 Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, 2 na kilima cha Hekalu 1 kitakuwa kichuguu 2 kilichofunikwa na vichaka.