Micah · Biblia (Kiswahili)

Micah 6

1Sikiliza asemalo Bwana: 1 “Simama, tetea shauri lako mbele ya milima; 2 vilima na visikie lile unalotaka kusema. 1

2Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana, 2 sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. 1 Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake; 2 anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. 1

3“Watu wangu, nimewatendea nini? 1 Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu. 1

4Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa 2 kutoka nchi ya utumwa. 1 Nilimtuma Mose awaongoze, 2 pia Aroni na Miriamu. 1

5Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu 2 alivyofanya shauri 2 na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. 1 Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali, 2 ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.” 1

6Nimjie Bwana na kitu gani na kusujudu 2 mbele za Mungu aliyetukuka? 1 Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa, 2 nije na ndama za mwaka mmoja? 1

7Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu, 2 au mito elfu kumi ya mafuta? 1 Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, 2 mtoto wangu mwenyewe 2 kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu? 1

8Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. 2 Bwana anataka nini kwako? 1 Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, 2 na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako. 1 Hatia Na Adhabu Ya Israeli 1

9Sikiliza! Bwana anauita mji: 2 kulicha jina lako ni hekima: 2 “Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru. 1

10Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu, 2 hazina yako uliyopata kwa udanganyifu 1 na vipimo vilivyopunguka, 2 ambavyo vimelaaniwa? 1

11Je, naweza kuhukumu kuwa 2 mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia, 2 aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo? 1

12Matajiri wake ni wajeuri; 2 watu wake ni waongo 1 na ndimi zao zinazungumza 2 kwa udanganyifu. 1

13Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu, 2 kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu. 1

14Mtakula lakini hamtashiba; 2 matumbo yenu bado yatakuwa matupu. 1 Mtaweka akiba lakini hamtaokoa chochote, 2 kwa sababu mtakachoweka akiba 2 nitatoa kwa upanga. 1

15Mtapanda lakini hamtavuna; 2 mtakamua zeituni lakini 2 hamtatumia mafuta yake. 1 Mtakamua zabibu 2 lakini hamtakunywa hiyo divai. 1

16Mmezishika sheria za Omri 2 na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, 2 tena umefuata desturi zao. 1 Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizi 2 na watu wako kuwa dhihaka; 2 mtachukua dharau za mataifa.”

← Micah 5Read In The App, Free →Micah 7 →

Study Micah 6

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567