Micah · Biblia (Kiswahili)

Micah 2

1Ole kwa wale wapangao uovu, 2 kwa wale wafanyao shauri la hila vitandani mwao! 1 Kunapopambazuka wanalitimiza 2 kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza. 1

2Wanatamani mashamba na kuyakamata, 2 pia nyumba na kuzichukua. 1 Wanamlaghai mwanaume nyumba yake, 2 mwanadamu mwenzake urithi wake.

3Kwa hiyo, Bwana asema: 1 “Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa, 2 ambayo hamwezi kujiokoa wenyewe. 1 Hamtatembea tena kwa majivuno, 2 kwa kuwa utakuwa ni wakati wa maafa. 1

4Siku hiyo watu watawadhihaki, 2 watawafanyia mzaha 2 kwa wimbo huu wa maombolezo: 1 ‘Tumeangamizwa kabisa; 2 mali ya watu wangu imegawanywa. 1 Ameninyangʼanya! 2 Ametoa mashamba yetu kwa wasaliti.’ ” 1

5Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la Bwana 2 wa kugawanya mashamba kwa kura. 1 Manabii Wa Uongo 1

6Manabii wao husema, “Usitabiri. 2 Usitabiri kuhusu vitu hivi; 2 aibu haitatupata.” 1

7Je, ingesemwa, ee nyumba ya Yakobo: 2 “Je, Roho wa Bwana amekasirika? 2 Je, yeye hufanya vitu kama hivyo?” 1 “Je, maneno yangu hayamfanyii mema 2 yeye ambaye njia zake ni nyofu? 1

8Siku hizi watu wangu wameinuka 2 kama adui. 1 Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita 2 pasipo kujali, 2 kama watu warudio kutoka vitani. 1

9Unawahamisha wanawake wa watu wangu 2 kutoka kwenye nyumba zao za kupendeza. 1 Unaondoa baraka yangu 2 kwa watoto wao milele. 1

10Inuka, nenda zako! 2 Kwa maana hapa sio mahali pako pa kupumzikia, 1 kwa sababu pametiwa unajisi, 2 pameharibiwa, wala hapatengenezeki tena. 1

11Ikiwa mwongo na mdanganyifu atakuja na kusema, 2 ‘Nitawatabiria divai na pombe kwa wingi,’ 1 angekuwa ndiye nabii 2 anayekubalika na watu hawa! 1 Ahadi Ya Ukombozi 1

12“Hakika nitawakusanya ninyi nyote, ee Yakobo, 2 Hakika nitawaleta pamoja mabaki ya Israeli. 1 Nitawaleta pamoja kama kondoo ndani ya zizi, 2 kama kundi kwenye malisho yake, 2 mahali hapa patakuwa na msongamano wa watu. 1

13Yeye afunguaye njia atawatangulia; 2 watapita kwenye lango na kutoka nje. 1 Mfalme wao atawatangulia, 2 Bwana atakuwa kiongozi.”

← Micah 1Read In The App, Free →Micah 3 →

Study Micah 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567