Micah · Biblia (Kiswahili)

Micah 5

1Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, 2 kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. 1 Watampiga mtawala wa Israeli 2 shavuni kwa fimbo. 1

2“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, 2 ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, 1 kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu 2 yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, 1 ambaye asili yake ni kutoka zamani, 2 kutoka milele.” 1

3Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati 2 mwanamke aliye na utungu atakapozaa 1 na ndugu zake wengine warudi 2 kujiunga na Waisraeli. 1

4Atasimama na kulichunga kundi lake 2 katika nguvu ya Bwana, 2 katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake. 1 Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo 2 ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia. 2

5Naye atakuwa amani yao. 1 Ukombozi Na Uharibifu 1 Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu 2 na kupita katika ngome zetu, 1 tutawainua wachungaji saba dhidi yake, 2 hata viongozi wanane wa watu. 1

6Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, 2 nchi ya Nimrodi kwa upanga. 1 Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru 2 atakapoivamia nchi yetu 2 na kuingia katika mipaka yetu. 1

7Mabaki ya Yakobo yatakuwa 2 katikati ya mataifa mengi 1 kama umande kutoka kwa Bwana, 2 kama manyunyu juu ya majani, 1 ambayo hayamngoji mtu 2 wala kukawia kwa mwanadamu. 1

8Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, 2 katikati ya mataifa mengi, 1 kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni, 2 kama mwana simba miongoni 2 mwa makundi ya kondoo, 1 ambaye anaumiza vibaya na kuwararua 2 kila anapopita katikati yao, 2 wala hakuna awezaye kuokoa. 1

9Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, 2 nao adui zako wote wataangamizwa.

10“Katika siku ile,” asema Bwana, 1 “nitaangamiza farasi zenu katikati yenu 2 na kubomoa magari yenu ya vita. 1

11Nitaiangamiza miji ya nchi yenu 2 na kuziangusha chini ngome zenu zote. 1

12Nitaangamiza uchawi wenu 2 na hamtapiga tena ramli. 1

13Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga 2 na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu; 1 hamtasujudia tena 2 kazi ya mikono yenu. 1

14Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenu 2 na kubomoa miji yenu. 1

15Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu 2 juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”

← Micah 4Read In The App, Free →Micah 6 →

Study Micah 5

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567