Song of Solomon · Biblia (Kiswahili)

Song of Solomon 1

1Wimbo ulio bora wa Solomoni. 1 Shairi La Kwanza Mpendwa 1

2Unibusu kwa busu la kinywa chako, 2 kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai. 1

3Manukato yako yananukia vizuri, 2 jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. 1 Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! 1

4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! 1 Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki 1 Tunakushangilia na kukufurahia, 1 tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa 1 Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! 1

5Mimi ni mweusi, lakini napendeza, 2 enyi binti za Yerusalemu, 2 mweusi kama mahema ya Kedari, 2 kama mapazia ya hema la Solomoni. 1

6Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, 2 kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. 1 Wana wa mama yangu walinikasirikia 2 na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. 2 Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. 1

7Niambie, wewe ambaye ninakupenda, 2 unalisha wapi kundi lako la kondoo 2 na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. 1 Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela 2 karibu na makundi ya rafiki zako? Marafiki 1

8Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, 2 fuata nyayo za kondoo, 1 na kulisha wana-mbuzi wako 2 karibu na hema za wachungaji. Mpenzi 1

9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike 2 aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. 1

10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, 2 shingo yako ikiwa na mikufu ya vito. 1

11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, 2 vyenye kupambwa kwa fedha. Mpendwa 1

12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake, 2 manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri. 1

13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane 2 kati ya matiti yangu. 1

14Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina 2 kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi. Mpenzi 1

15Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! 2 Tazama jinsi ulivyo mzuri! 2 Macho yako ni kama ya hua. Mpendwa 1

16Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! 2 Ee, tazama jinsi unavyopendeza! 2 Na kitanda chetu ni cha majani mazuri. Mpenzi 1

17Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, 2 na mapao yetu ni miberoshi.

← Ecclesiastes 12Read In The App, Free →Song of Solomon 2 →

Study Song of Solomon 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678