Song of Solomon 3
1Usiku kucha kwenye kitanda changu 2 nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; 2 nilimtafuta, lakini sikumpata. 1
2Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, 2 katika barabara zake na viwanja; 1 nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. 2 Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. 1
3Walinzi walinikuta 2 walipokuwa wakizunguka mji. 1 Nikawauliza, “Je, mmemwona 2 yule moyo wangu umpendaye?” 1
4Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita 2 nilimpata yule moyo wangu umpendaye. 1 Nilimshika na sikumwachia aende 2 mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, 2 katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. 1
5Binti za Yerusalemu, ninawaagiza 2 kwa paa na kwa ayala wa shambani: 1 Msichochee wala kuamsha mapenzi 2 hata yatakapotaka yenyewe. 1 Shairi La Tatu Mpenzi 1
6Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani 2 kama nguzo ya moshi, 1 anayenukia manemane na uvumba 2 iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote 2 vya mfanyabiashara? 1
7Tazama! Ni gari la Solomoni 2 lisindikizwalo na mashujaa sitini, 2 walio wakuu sana wa Israeli, 1
8wote wamevaa panga, 2 wote wazoefu katika vita, 1 kila mmoja na upanga wake pajani, 2 wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku. 1
9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; 2 alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni. 1
10Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, 2 kitako chake kwa dhahabu. 1 Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, 2 gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo 2 na binti za Yerusalemu. 1
11Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, 2 mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji, 1 taji ambalo mama yake alimvika 2 siku ya arusi yake, 2 siku ambayo moyo wake ulishangilia.