Song of Solomon 5
1Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, 2 bibi arusi wangu; 1 nimekusanya manemane yangu pamoja 2 na kikolezo changu. 1 Nimekula sega langu la asali na asali yangu; 2 nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Marafiki 1 Kuleni, enyi marafiki, mnywe; 1 kunyweni ya kutosha, ee wapenzi. 1 Shairi La Nne Mpendwa 1
2Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. 1 Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: 2 “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, 2 hua wangu, asiye na hitilafu. 1 Kichwa changu kimeloa umande, 2 na nywele zangu manyunyu ya usiku.” 1
3Nimevua joho langu: 2 je, ni lazima nivae tena? 1 Nimenawa miguu yangu: 2 je, ni lazima niichafue tena? 1
4Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo; 2 moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake. 1
5Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu, 2 mikono yangu ikidondosha manemane, 1 vidole vyangu vikitiririka manemane, 2 penye vipini vya komeo. 1
6Nilimfungulia mpenzi wangu, 2 lakini mpenzi wangu alishaondoka; 2 alikuwa amekwenda zake. 1 Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake. 2 Nilimtafuta lakini sikumpata. 2 Nilimwita lakini hakunijibu. 1
7Walinzi walinikuta 2 walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini. 1 Walinipiga, wakanijeruhi, 2 wakaninyangʼanya joho langu, 2 hao walinzi wa kuta! 1
8Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza: 2 kama mkimpata mpenzi wangu, 1 mtamwambia nini? 2 Mwambieni ninazimia kwa mapenzi. Marafiki 1
9Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani, 2 wewe uliye mzuri kupita wanawake wote? 1 Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani, 2 hata unatuagiza hivyo? Mpendwa 1
10Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu, 2 wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu. 1
11Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote, 2 nywele zake ni za mawimbi 2 na ni nyeusi kama kunguru. 1
12Macho yake ni kama ya hua 2 kandokando ya vijito vya maji, 1 aliyeogeshwa kwenye maziwa, 2 yaliyopangwa kama vito vya thamani. 1
13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo 2 yakitoa manukato. 1 Midomo yake ni kama yungiyungi 2 inayodondosha manemane. 1
14Mikono yake ni fimbo za dhahabu 2 iliyopambwa kwa krisolitho. 1 Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa 2 iliyopambwa na yakuti samawi. 1
15Miguu yake ni nguzo za marmar 2 zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi. 1 Sura yake ni kama Lebanoni, 2 bora kama miti yake ya mierezi. 1
16Kinywa chake chenyewe ni utamu, 2 kwa ujumla yeye ni wa kupendeza. 1 Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu, 2 ee binti za Yerusalemu.