Song of Solomon 2
1Mimi ni ua la Sharoni, 2 yungiyungi ya bondeni. Mpenzi 1
2Kama yungiyungi katikati ya miiba 2 ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali. Mpendwa 1
3Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni 2 ndivyo alivyo mpenzi wangu 2 miongoni mwa wanaume vijana. 1 Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, 2 na tunda lake ni tamu kwangu. 1
4Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu, 2 na bendera ya huyu mwanaume 2 juu yangu ni upendo. 1
5Nitie nguvu kwa zabibu kavu, 2 niburudishe kwa matofaa, 2 kwa maana ninazimia kwa mapenzi. 1
6Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, 2 na mkono wake wa kuume unanikumbatia. 1
7Binti za Yerusalemu, ninawaagiza 2 kwa paa na kwa ayala wa shambani: 1 Msichochee wala kuamsha mapenzi 2 hata yatakapotaka yenyewe. 1 Shairi La Pili Mpendwa 1
8Sikiliza! Mpenzi wangu! 2 Tazama! Huyu hapa anakuja, 1 akirukaruka juu milimani 2 akizunguka juu ya vilima. 1
9Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana. 2 Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu, 1 akitazama kupitia madirishani, 2 akichungulia kimiani. 1
10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, 2 “Inuka, mpenzi wangu, 2 mrembo wangu, tufuatane. 1
11Tazama! Wakati wa masika umepita, 2 mvua imekwisha na ikapita. 1
12Maua yanatokea juu ya nchi; 2 majira ya kuimba yamewadia, 1 sauti za njiwa zinasikika 2 katika nchi yetu. 1
13Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, 2 zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. 1 Inuka, njoo mpenzi wangu. 2 Mrembo wangu, tufuatane.” Mpenzi 1
14Hua wangu penye nyufa za majabali, 2 mafichoni pembezoni mwa mlima, 1 nionyeshe uso wako, 2 na niisikie sauti yako, 1 kwa maana sauti yako ni tamu, 2 na uso wako unapendeza. 1
15Tukamatie mbweha, 2 mbweha wale wadogo 1 wanaoharibu mashamba ya mizabibu, 2 mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua. Mpendwa 1
16Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, 2 yeye hujilisha katikati ya yungiyungi. 1
17Mpaka jua linapochomoza, 2 na vivuli vikimbie, 1 rudi, mpenzi wangu, 2 na uwe kama paa, 1 au kama ayala kijana 2 juu ya vilima vya Betheri.