Song of Solomon · Biblia (Kiswahili)

Song of Solomon 7

1Ee binti wa mwana wa mfalme, 2 tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu! 1 Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani, 2 kazi ya mikono ya fundi stadi. 1

2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo 2 ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa. 1 Kiuno chako ni kichuguu cha ngano 2 kilichozungukwa kwa yungiyungi. 1

3Matiti yako ni kama wana-paa wawili, 2 mapacha wa paa. 1

4Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu. 2 Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni 2 karibu na lango la Beth-Rabi. 1 Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni 2 ukitazama kuelekea Dameski. 1

5Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli. 2 Nywele zako ni kama zulia la urujuani; 2 mfalme ametekwa na mashungi yake. 1

6Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza, 2 ee pendo, kwa uzuri wako! 1

7Umbo lako ni kama la mtende, 2 nayo matiti yako kama vishada vya matunda. 1

8Nilisema, “Nitakwea mtende, 2 nami nitayashika matunda yake.” 1 Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, 2 harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa, 1

9na kinywa chako kama divai 2 bora kuliko zote. Mpendwa 1 Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu, 2 ikitiririka polepole juu ya midomo na meno. 1

10Mimi ni mali ya mpenzi wangu, 2 nayo shauku yake ni juu yangu. 1

11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, 2 twende tukalale huko vijijini. 1

12Hebu na twende mapema 2 katika mashamba ya mizabibu 2 tuone kama mizabibu imechipua, 1 kama maua yake yamefunguka, 2 na kama mikomamanga imetoa maua: 2 huko nitakupa penzi langu. 1

13Mitunguja hutoa harufu zake nzuri, 2 kwenye milango yetu kuna matunda mazuri, 1 mapya na ya zamani, 2 ambayo nimekuhifadhia wewe, 2 mpenzi wangu.

← Song of Solomon 6Read In The App, Free →Song of Solomon 8 →

Study Song of Solomon 7

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678