Song of Solomon 4
1Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! 2 Ee, jinsi ulivyo mzuri! 1 Macho yako nyuma ya shela yako 2 ni kama ya hua. 1 Nywele zako ni kama kundi la mbuzi 2 zikishuka kutoka Mlima Gileadi. 1
2Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi, 2 watokao kuogeshwa. 1 Kila mmoja ana pacha lake, 2 hakuna hata mmoja aliye peke yake. 1
3Midomo yako ni kama uzi mwekundu, 2 kinywa chako kinapendeza. 1 Mashavu yako nyuma ya shela yako 2 ni kama vipande viwili vya komamanga. 1
4Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, 2 uliojengwa kwa madaha, 1 juu yake zimetundikwa ngao elfu, 2 zote ni ngao za mashujaa. 1
5Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili, 2 kama wana-paa mapacha 2 wajilishao katikati ya yungiyungi. 1
6Hata kupambazuke na vivuli vikimbie, 2 nitakwenda kwenye mlima wa manemane 2 na kwenye kilima cha uvumba. 1
7Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, 2 hakuna hitilafu ndani yako. 1
8Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, 2 enda nami kutoka Lebanoni. 1 Shuka kutoka ncha ya Amana, 2 kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, 1 kutoka mapango ya simba 2 na kutoka mlima wapendapo kukaa chui. 1
9Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; 2 umeiba moyo wangu 1 kwa mtazamo mmoja wa macho yako, 2 kwa kito kimoja cha mkufu wako. 1
10Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, 2 dada yangu, bibi arusi wangu! 1 Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, 2 na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote! 1
11Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, 2 bibi arusi wangu; 1 maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. 2 Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni. 1
12Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, 2 bibi arusi wangu; 1 wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, 2 chemchemi yangu peke yangu. 1
13Mimea yako ni bustani ya mikomamanga 2 yenye matunda mazuri sana, 2 yenye hina na nardo, 1
14nardo na zafarani, 2 mchai na mdalasini, 2 pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, 2 manemane na udi, 2 na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote. 1
15Wewe ni chemchemi ya bustani, 2 kisima cha maji yatiririkayo, 2 yakitiririka kutoka Lebanoni. Mpendwa 1
16Amka, upepo wa kaskazini, 2 na uje, upepo wa kusini! 2 Vuma juu ya bustani yangu, 2 ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo. 1 Mpendwa wangu na aje bustanini mwake 2 na kuonja matunda mazuri sana.