Song of Solomon · Biblia (Kiswahili)

Song of Solomon 6

1Mpenzi wako amekwenda wapi, 2 ewe mzuri kupita wanawake wote? 1 Mpenzi wako amegeukia njia ipi, 2 tupate kumtafuta pamoja nawe? Mpendwa 1

2Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake, 2 kwenye vitalu vya vikolezo, 1 kujilisha bustanini 2 na kukusanya yungiyungi. 1

3Mimi ni wake mpenzi wangu, 2 na mpenzi wangu ni wangu; 2 yeye hujilisha katikati ya yungiyungi. 1 Shairi La Tano Mpenzi 1

4Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa, 2 upendezaye kama Yerusalemu, 2 umetukuka kama jeshi lenye bendera. 1

5Uyageuze macho yako mbali nami, 2 yananigharikisha. 1 Nywele zako ni kama kundi la mbuzi 2 wanaoteremka kutoka Gileadi. 1

6Meno yako ni kama kundi la kondoo 2 watokao kuogeshwa. 1 Kila mmoja ana pacha lake, 2 hakuna hata mmoja aliye peke yake. 1

7Mashavu yako nyuma ya shela yako 2 ni kama vipande viwili vya komamanga. 1

8Panaweza kuwepo malkia sitini, 2 masuria themanini 2 na mabikira wasiohesabika; 1

9lakini hua wangu, mkamilifu wangu, 2 ni wa namna ya pekee, 1 binti pekee kwa mama yake, 2 kipenzi cha yeye aliyemzaa. 1 Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa; 2 malkia na masuria walimsifu. Marafiki 1

10Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko, 2 mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, 2 ametukuka kama nyota zifuatanazo? Mpenzi 1

11Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi 2 ili kutazama machipuko ya bondeni, 1 kuona kama mizabibu imechipua 2 au kama mikomamanga imechanua maua. 1

12Kabla sijangʼamua, 2 shauku yangu iliniweka 2 katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu. Marafiki 1

13Rudi, rudi, ee Mshulami; 2 rudi, rudi ili tupate kukutazama! Mpenzi 1 Kwa nini kumtazama Mshulami, 2 kama kutazama ngoma ya Mahanaimu? + 6:13 Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili.

← Song of Solomon 5Read In The App, Free →Song of Solomon 7 →

Study Song of Solomon 6

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678