Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 10

1Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, 2 alijizalia matunda mwenyewe. 1 Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, 2 alijenga madhabahu zaidi; 1 kadiri nchi yake ilivyostawi, 2 alipamba mawe yake ya ibada. 1

2Moyo wao ni mdanganyifu, 2 nao sasa lazima wachukue hatia yao. 1 Bwana atabomoa madhabahu zao 2 na kuharibu mawe yao ya ibada. 1

3Kisha watasema, “Hatuna mfalme 2 kwa sababu hatukumheshimu Bwana. 1 Lakini hata kama tungelikuwa na mfalme, 2 angeweza kutufanyia nini?” 1

4Wanaweka ahadi nyingi, 2 huapa viapo vya uongo 2 wanapofanya mapatano; 1 kwa hiyo mashtaka huchipuka 2 kama magugu ya sumu 2 katika shamba lililolimwa. 1

5Watu wanaoishi Samaria huogopa 2 kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni. + 10:5 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka. 1 Watu wake wataiombolezea, 2 vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu, 1 wale waliokuwa wamefurahia fahari yake, 2 kwa sababu itaondolewa kutoka kwao 2 kwenda uhamishoni. 1

6Itachukuliwa kwenda Ashuru 2 kama ushuru kwa mfalme mkuu. 1 Efraimu atafedheheshwa; 2 Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti. 1

7Samaria na mfalme wake wataelea 2 kama kijiti juu ya uso wa maji. 1

8Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu + 10:8 Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni , jina lingine la Betheli kwa dhihaka. pataharibiwa: 2 ndiyo dhambi ya Israeli. 1 Miiba na mibaruti itaota 2 na kufunika madhabahu zao. 1 Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” 2 na vilima, “Tuangukieni!” 1

9“Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli, 2 huko ndiko mlikobaki. 1 Je, vita havikuwapata 2 watenda mabaya huko Gibea? 1

10Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu; 2 mataifa yatakusanywa dhidi yao 1 ili kuwaweka katika vifungo 2 kwa ajili ya dhambi zao mbili. 1

11Efraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwa 2 ambaye hupenda kupura, 1 hivyo nitamfunga nira 2 juu ya shingo yake nzuri. 1 Nitamwendesha Efraimu, 2 Yuda lazima alime, 1 naye Yakobo lazima avunjavunje 2 mabonge ya udongo. 1

12Jipandieni wenyewe haki, 2 vuneni matunda ya upendo usio na kikomo, 1 vunjeni ardhi yenu isiyolimwa; 2 kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana, 1 mpaka atakapokuja 2 na kuwanyeshea juu yenu haki. 1

13Lakini mmepanda uovu, 2 mkavuna ubaya, 2 mmekula tunda la udanganyifu. 1 Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe 2 na wingi wa mashujaa wenu, 1

14mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako, 2 ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa: 1 kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita, 2 wakati mama pamoja na watoto wao 2 walipotupwa kwa nguvu ardhini. 1

15Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli, 2 kwa sababu uovu wako ni mkuu. 1 Siku ile itakapopambazuka, 2 mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa.

← Hosea 9Read In The App, Free →Hosea 11 →

Study Hosea 10

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314