Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 6

1“Njooni, tumrudie Bwana. 1 Ameturarua vipande vipande 2 lakini atatuponya; 1 ametujeruhi lakini 2 atatufunga majeraha yetu. 1

2Baada ya siku mbili atatufufua; 2 katika siku ya tatu atatuinua, 2 ili tuweze kuishi mbele zake. 1

3Tumkubali Bwana, 2 tukaze kumkubali yeye. 1 Kutokea kwake ni hakika kama vile 2 kuchomoza kwa jua; 1 atatujia kama mvua za masika, 2 kama vile mvua za vuli 2 ziinyweshavyo nchi.” 1

4“Nifanye nini nawe, Efraimu? 2 Nifanye nini nawe, Yuda? 1 Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi, 2 kama umande wa alfajiri utowekao. 1

5Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande 2 kwa kutumia manabii wangu; 1 nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu, 2 hukumu zangu zinawaka 2 kama umeme juu yenu. 1

6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu, 2 kumkubali Mungu zaidi 2 kuliko sadaka za kuteketezwa. 1

7Wamevunja Agano kama Adamu: 2 huko hawakuwa waaminifu kwangu. 1

8Gileadi ni mji wenye watu waovu, 2 umetiwa madoa kwa nyayo za damu. 1

9Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu, 2 ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; 1 wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, 2 wakifanya uhalifu wa aibu. 1

10Nimeona jambo la kutisha 2 katika nyumba ya Israeli. 1 Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba 2 na Israeli amenajisika. 1

11“Pia kwa ajili yako, Yuda, 2 mavuno yameamriwa. 1 “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

← Hosea 5Read In The App, Free →Hosea 7 →

Study Hosea 6

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314