Hosea 4
1Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli, 2 kwa sababu Bwana analo shtaka 2 dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: 1 “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, 2 hakuna kumjua Mungu katika nchi. 1
2Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, 2 wizi na uzinzi, 1 bila kuwa na mipaka, 2 nao umwagaji damu mmoja 2 baada ya mwingine. 1
3Kwa sababu hii nchi huomboleza, 2 wote waishio ndani mwake wanadhoofika, 1 wanyama wa kondeni, ndege wa angani 2 na samaki wa baharini wanakufa. 1
4“Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka, 2 mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, 1 kwa maana watu wako ni kama wale 2 waletao mashtaka dhidi ya kuhani. 1
5Unajikwaa usiku na mchana, 2 nao manabii hujikwaa pamoja nawe. 1 Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako: 2
6watu wangu wanaangamizwa 2 kwa kukosa maarifa, 1 “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, 2 mimi nami nitakukataa wewe 2 usiwe kuhani kwangu mimi; 1 kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako 2 mimi nami sitawajali watoto wako. 1
7Kadiri makuhani walivyoongezeka, 2 ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu, 2 walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu. 1
8Hujilisha dhambi za watu wangu 2 na kupendezwa na uovu wao. 1
9Hata itakuwa: Kama walivyo watu, 2 ndivyo walivyo makuhani. 1 Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao 2 na kuwalipa kwa matendo yao. 1
10“Watakula lakini hawatashiba; 2 watajiingiza katika ukahaba 2 lakini hawataongezeka, 1 kwa sababu wamemwacha Bwana 2 na kujiingiza wenyewe 2
11katika ukahaba, 1 divai ya zamani na divai mpya, 2 ambavyo huondoa ufahamu 2
12wa watu wangu. 1 Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti 2 nao hujibiwa na fimbo ya mti. 1 Roho ya ukahaba imewapotosha, 2 hawana uaminifu kwa Mungu wao. 1
13Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima 2 na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima, 1 chini ya mialoni, milibua na miela, 2 ambako kuna vivuli vizuri. 1 Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba 2 na wake za wana wenu uzinzi. 1
14“Sitawaadhibu binti zenu wakati 2 wanapogeukia ukahaba, 1 wala wake za wana wenu 2 wanapofanya uzinzi, 1 kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya 2 na kutambikia pamoja na makahaba 2 wa mahali pa kuabudia miungu: 1 watu wasiokuwa na ufahamu 2 wataangamia! 1
15“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, 2 Yuda naye asije akawa na hatia. 1 “Usiende Gilgali, 2 usipande kwenda Beth-Aveni + 4:15 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka. 1 Wala usiape, 2 ‘Hakika kama Bwana aishivyo!’ 1
16Waisraeli ni wakaidi, 2 kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi. 1 Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga 2 kama wana-kondoo 2 katika shamba la majani? 1
17Efraimu amejiunga na sanamu, 2 ondokana naye! 1
18Hata wakati wamemaliza vileo vyao 2 wanaendelea na ukahaba wao, 1 watawala wao hupenda sana 2 njia za aibu. 1
19Kisulisuli kitawafagilia mbali 2 na dhabihu zao zitawaletea aibu.