Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 11

1“Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda, 2 nilimwita mwanangu kutoka Misri. 1

2Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, 2 ndivyo walivyokwenda mbali nami. 1 Walitoa dhabihu kwa Mabaali 2 na kufukiza uvumba kwa vinyago. 1

3Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, 2 nikiwashika mikono; 1 lakini hawakutambua 2 kuwa ni mimi niliyewaponya. 1

4Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, 2 kwa vifungo vya upendo; 1 niliondoa nira shingoni mwao 2 nami nikainama kuwalisha. 1

5“Je, hawatarudi Misri, 2 nayo Ashuru haitawatawala 2 kwa sababu wamekataa kutubu? 1

6Panga zitametameta katika miji yao, 2 zitaharibu makomeo ya malango yao 2 na kukomesha mipango yao. 1

7Watu wangu wamedhamiria kuniacha. 2 Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana, 2 kwa vyovyote hatawainua. 1

8“Efraimu, ninawezaje kukuacha? 2 Ee Israeli, ninawezaje kukutoa? 1 Nitawezaje kukutendea kama Adma? 2 Nitawezaje kukufanya kama Seboimu? 1 Moyo wangu umegeuka ndani yangu, 2 huruma zangu zote zimeamshwa. 1

9Sitatimiza hasira yangu kali, 2 wala sitageuka na kumharibu Efraimu. 1 Kwa kuwa mimi ndimi Mungu, 2 wala si mwanadamu, 1 Aliye Mtakatifu miongoni mwenu. 2 Sitakuja kwa ghadhabu. 1

10Watamfuata Bwana; 2 atanguruma kama simba. 1 Wakati angurumapo, 2 watoto wake watakuja wakitetemeka 2 kutoka magharibi. 1

11Watakuja wakitetemeka 2 kama ndege wakitoka Misri, 2 kama hua wakitoka Ashuru. 1 Nitawakalisha katika nyumba zao,” 2 asema Bwana. 1 Dhambi Ya Israeli 1

12Efraimu amenizunguka kwa uongo, 2 nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. 1 Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu, 2 hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.

← Hosea 10Read In The App, Free →Hosea 12 →

Study Hosea 11

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314