Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 7

1kila mara nilipotaka kumponya Israeli, 2 dhambi za Efraimu zinafichuliwa 2 na maovu ya Samaria yanafunuliwa. 1 Wanafanya udanganyifu, 2 wevi huvunja nyumba, 2 maharamia hunyangʼanya barabarani, 1

2lakini hawafahamu kwamba 2 ninakumbuka matendo yao yote mabaya. 1 Dhambi zao zimewameza, 2 ziko mbele zangu siku zote. 1

3“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao, 2 wakuu wao kwa uongo wao. 1

4Wote ni wazinzi, 2 wanawaka kama tanuru 1 ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea 2 kuanzia kukanda unga 2 hadi umekwisha kuumuka. 1

5Katika sikukuu ya mfalme wetu 2 wakuu wanawaka kwa mvinyo, 2 naye anawaunga mkono wenye mizaha. 1

6Mioyo yao ni kama tanuru, 2 wanamwendea kwa hila. 1 Hasira yao inafoka moshi usiku kucha, 2 wakati wa asubuhi inalipuka 2 kama miali ya moto. 1

7Wote ni moto kama tanuru; 2 wanawaangamiza watawala wao. 1 Wafalme wake wote wanaanguka, 2 wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi. 1

8“Efraimu anajichanganya na mataifa; 2 Efraimu ni mkate ambao haukuiva. 1

9Wageni wananyonya nguvu zake, 2 lakini hafahamu hilo. 1 Nywele zake zina mvi hapa na pale, 2 lakini hana habari. 1

10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake, 2 lakini pamoja na haya yote 1 harudi kwa Bwana Mungu wake 2 wala kumtafuta. 1

11“Efraimu ni kama hua, 2 hudanganywa kwa urahisi na hana akili: 1 mara anaita Misri, 2 mara anageukia Ashuru. 1

12Wakati watakapokwenda, 2 nitatupa wavu wangu juu yao; 1 nitawavuta chini waanguke 2 kama ndege wa angani. 1 Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, 2 nitawanasa. 1

13Ole wao, kwa sababu 2 wamepotoka kutoka kwangu! 1 Maangamizi ni yao 2 kwa sababu wameniasi! 1 Ninatamani kuwakomboa, 2 lakini wanasema uongo dhidi yangu. 1

14Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao, 2 bali wanaomboleza vitandani mwao. 1 Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, 2 lakini hugeukia mbali nami. 1

15Niliwafundisha na kuwatia nguvu, 2 lakini wanapanga mabaya dhidi yangu. 1

16Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana, 2 wako kama upinde wenye kasoro. 1 Viongozi wao wataanguka kwa upanga 2 kwa sababu ya maneno yao ya jeuri. 1 Kwa ajili ya hili watadhihakiwa 2 katika nchi ya Misri.

← Hosea 6Read In The App, Free →Hosea 8 →

Study Hosea 7

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314