Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 12

1Efraimu anajilisha upepo; 2 hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima 2 na kuzidisha uongo na jeuri. 1 Anafanya mkataba na Ashuru 2 na kutuma mafuta ya zeituni Misri. 1

2Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda, 2 atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake 2 na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake. 1

3Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake; 2 kama mwanadamu, alishindana na Mungu. 1

4Alishindana na malaika na kumshinda; 2 alilia na kuomba upendeleo wake. 1 Alimkuta huko Betheli 2 na kuzungumza naye huko: 1

5Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, 2 Bwana ndilo jina lake! 1

6Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako; 2 dumisha upendo na haki, 2 nawe umngojee Mungu wako siku zote. 1

7Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu; 2 hupenda kupunja. 1

8Efraimu hujisifu akisema, 2 “Mimi ni tajiri sana; nimetajirika. 1 Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu 2 uovu wowote au dhambi.” 1

9“Mimi ndimi Bwana Mungu wenu 2 niliyewaleta kutoka Misri; 1 nitawafanya mkae tena kwenye mahema, 2 kama vile katika siku 2 za sikukuu zenu zilizoamriwa. 1

10Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi 2 na kusema mifano kupitia wao.” 1

11Je, Gileadi si mwovu? 2 Watu wake hawafai kitu! 1 Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali? 2 Madhabahu zao zitakuwa 2 kama malundo ya mawe 2 katika shamba lililolimwa. 1

12Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu; 2 Israeli alitumika ili apate mke, 2 ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo. 1

13Bwana alimtumia nabii 2 kumpandisha Israeli kutoka Misri, 2 kwa njia ya nabii alimtunza. 1

14Lakini Efraimu amemchochea sana hasira; 2 Bwana wake ataleta juu yake 1 hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza 2 kwa ajili ya dharau yake.

← Hosea 11Read In The App, Free →Hosea 13 →

Study Hosea 12

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314