Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 9

1Usifurahie, ee Israeli; 2 usishangilie kama mataifa mengine. 1 Kwa kuwa hukuwa 2 mwaminifu kwa Mungu wako; 1 umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu 2 ya kupuria nafaka. 1

2Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divai 2 havitalisha watu, 2 divai mpya itawapungukia. 1

3Hawataishi katika nchi ya Bwana, 2 Efraimu atarudi Misri 1 na atakula chakula 2 kilicho najisi huko Ashuru. 1

4Hawatammiminia Bwana sadaka ya divai 2 wala dhabihu zao hazitampendeza. 1 Dhabihu kama hizo zitakuwa kwao 2 kama mkate wa waombolezaji; 2 nao wote wazilao watakuwa najisi. 1 Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe; 2 kisije katika Hekalu la Bwana. 1

5Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, 2 katika siku za sikukuu za Bwana? 1

6Hata ikiwa wataokoka maangamizi, 2 Misri atawakusanya, 2 nayo Memfisi + 9:6 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. itawazika. 1 Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma, 2 nayo miiba itafunika mahema yao. 1

7Siku za adhabu zinakuja, 2 siku za malipo zimewadia. 2 Israeli na afahamu hili. 1 Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana 2 na uadui wenu ni mkubwa sana, 1 nabii anadhaniwa ni mpumbavu, 2 mtu aliyeongozwa na Mungu 2 anaonekana mwendawazimu. 1

8Nabii, pamoja na Mungu wangu, 2 ndiye mlinzi juu ya Efraimu, 1 hata hivyo mitego inamngojea 2 katika mapito yake yote, 2 na uadui katika nyumba ya Mungu wake. 1

9Wamezama sana katika rushwa, 2 kama katika siku za Gibea. 1 Mungu atakumbuka uovu wao 2 na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao. 1

10“Nilipompata Israeli, ilikuwa kama 2 kupata zabibu jangwani; 1 nilipowaona baba zenu, ilikuwa kama kuona 2 matunda ya kwanza katika mtini. 1 Lakini walipofika Baal-Peori, walijiweka wakfu 2 kwa ile sanamu ya aibu, 1 nao wakawa najisi 2 kama kitu kile walichokipenda. 1

11Utukufu wa Efraimu utaruka kama ndege: 2 hakuna kuzaa, hakuna kuchukua mimba, 2 hakuna kutunga mimba. 1

12Hata wakilea watoto, 2 nitamuua kila mmoja. 1 Ole wao 2 nitakapowapiga kisogo! 1

13Nimemwona Efraimu, kama Tiro, 2 aliyeoteshwa mahali pazuri. 1 Lakini Efraimu wataleta 2 watoto wao kwa mchinjaji.” 1

14Wape, Ee Bwana, 2 je, utawapa nini? 1 Wape matumbo ya kuharibu mimba 2 na matiti yaliyokauka. 1

15“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali, 2 niliwachukia huko. 1 Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi, 2 nitawafukuza katika nyumba yangu. 1 Sitawapenda tena, 2 viongozi wao wote ni waasi. 1

16Efraimu ameharibiwa, 2 mzizi wao umenyauka, 2 hawazai tunda. 1 Hata kama watazaa watoto, 2 nitawachinja watoto wao 2 waliotunzwa vizuri.” 1

17Mungu wangu atawakataa 2 kwa sababu hawakumtii; 1 watakuwa watu wa kutangatanga 2 miongoni mwa mataifa.

← Hosea 8Read In The App, Free →Hosea 10 →

Study Hosea 9

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314