Hosea 5
1“Sikieni hili, enyi makuhani! 2 Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli! 1 Sikieni, ee nyumba ya mfalme! 2 Hukumu hii ni dhidi yenu: 1 Mmekuwa mtego huko Mispa, 2 wavu uliotandwa juu ya Tabori. 1
2Waasi wamezidisha sana mauaji. 2 Mimi nitawatiisha wote. 1
3Ninajua yote kuhusu Efraimu, 2 Israeli hukufichika kwangu. 1 Efraimu, sasa umegeukia ukahaba, 2 Israeli amenajisika. 1
4“Matendo yao hayawaachii 2 kurudi kwa Mungu wao. 1 Roho ya ukahaba imo ndani ya mioyo yao, 2 hawamkubali Bwana. 1
5Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao; 2 Waisraeli, hata Efraimu, 1 wanajikwaa katika dhambi zao; 2 pia Yuda atajikwaa pamoja nao. 1
6Wakati wanapokwenda na makundi yao 2 ya kondoo na ngʼombe 2 kumtafuta Bwana, 1 hawatampata; 2 yeye amejiondoa kutoka kwao. 1
7Wao si waaminifu kwa Bwana; 2 wamezaa watoto haramu. 1 Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi 2 zitawaangamiza wao 2 pamoja na mashamba yao. 1
8“Pigeni tarumbeta huko Gibea, 2 baragumu huko Rama. 1 Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni, + 5:8 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka. 2 ongoza, ee Benyamini. 1
9Efraimu ataachwa ukiwa 2 katika siku ya kuadhibiwa. 1 Miongoni mwa makabila ya Israeli 2 ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia. 1
10Viongozi wa Yuda ni kama wale 2 wanaosogeza mawe ya mpaka. 1 Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao 2 kama mafuriko ya maji. 1
11Efraimu ameonewa, 2 amekanyagwa katika hukumu 2 kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu. 1
12Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, 2 na kama uozo kwa watu wa Yuda. 1
13“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake, 2 naye Yuda vidonda vyake, 1 ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru, 2 na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. 1 Lakini hawezi kukuponya, 2 wala hawezi kukuponya vidonda vyako. 1
14Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu, 2 kama simba mkubwa kwa Yuda. 1 Nitawararua vipande vipande na kuondoka; 2 nitawachukua mbali, 2 na hakuna wa kuwaokoa. 1
15Kisha nitarudi mahali pangu 2 mpaka watakapokubali kosa lao. 1 Nao watautafuta uso wangu; 2 katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”