Hosea 2
1“Waambie ndugu zako, ‘Watu wangu,’ na pia waambie dada zako, ‘Wapendwa wangu.’ 1 Israeli Aadhibiwa Na Kurudishwa 1
2“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni, 2 kwa maana yeye si mke wangu, 2 nami si mume wake. 1 Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake 2 na uzinzi kati ya matiti yake. 1
3Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi 2 na kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa. 1 Nitamfanya kama jangwa, 2 nitamgeuza awe nchi ya kiu, 2 nami nitamuua kwa kiu. 1
4Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake, 2 kwa sababu ni watoto wa uzinzi. 1
5Mama yao amekosa uaminifu 2 na amewachukua mimba katika aibu. 1 Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu, 2 ambao hunipa chakula changu 2 na maji yangu, 1 sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu 2 na kinywaji changu.’ 1
6Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake 2 kwa vichaka vya miiba, 1 nitamjengea ukuta ili kwamba 2 asiweze kutoka. 1
7Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata; 2 atawatafuta lakini hatawapata. 1 Kisha atasema, 2 ‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza, 1 kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi 2 kuliko sasa.’ 1
8Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiye 2 niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta, 1 niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumia 2 kwa kumtumikia Baali. 1
9“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa 2 na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari. 1 Nitamnyangʼanya sufu yangu na kitani yangu 2 iliyokusudiwa kufunika uchi wake. 1
10Basi sasa nitaufunua ufisadi wake 2 mbele ya wapenzi wake; 1 hakuna yeyote atakayemtoa 2 mikononi mwangu. 1
11Nitakomesha furaha na macheko yake yote: 2 sikukuu zake za mwaka, 2 sikukuu za Miandamo ya Mwezi, 2 siku zake za Sabato, 2 sikukuu zake zote zilizoamriwa. 1
12Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, 2 ambayo alisema yalikuwa malipo yake 2 kutoka kwa wapenzi wake; 1 nitaifanya kuwa kichaka, 2 nao wanyama pori wataila. 1
13Nitamwadhibu kwa ajili ya siku 2 alizowafukizia uvumba Mabaali; 1 alipojipamba kwa pete 2 na kwa vito vya thamani, 1 na kuwaendea wapenzi wake, 2 lakini mimi alinisahau,” 4 asema Bwana. 1
14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi; 2 nitamwongoza hadi jangwani 2 na kuzungumza naye kwa upole. 1
15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu, 2 nami nitalifanya Bonde la Akori + 2:15 Akori maana yake ni Taabu. 2 mlango wa matumaini. 1 Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake, 2 kama siku zile alizotoka Misri. 1
16“Katika siku ile,” asema Bwana, 2 “utaniita mimi ‘Mume wangu’; 2 hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’ 1
17Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake, 2 wala hataomba tena kwa majina yao. 1
18Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao 2 na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani, 2 na viumbe vile vitambaavyo ardhini. 1 Upinde, upanga na vita, 2 nitaondolea mbali katika nchi, 2 ili kwamba wote waweze kukaa salama. 1
19Nitakuposa uwe wangu milele; 2 nitakuposa kwa uadilifu na haki, 2 kwa upendo na huruma. 1
20Nitakuposa kwa uaminifu, 2 nawe utamkubali Bwana. 1
21“Katika siku ile nitajibu,” 2 asema Bwana, 1 “nitajibu kwa anga, 2 nazo anga zitajibu kwa nchi; 1
22nayo nchi itajibu kwa nafaka, 2 divai mpya na mafuta, 2 navyo vitajibu kwa Yezreeli. 1
23Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; 2 nami nitaonyesha pendo langu kwake 2 yule ambaye nilimwita, ‘Si mpenzi wangu. + 2:23 Kiebrania ni Lo-Ruhama.’ 1 Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio watu wangu,’ + 2:23 Kiebrania ni Lo-Ami. 2 ‘Ninyi ni watu wangu’; 2 nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu.’ ”