Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 8

1“Wekeni tarumbeta midomoni mwenu! 2 Tai yuko juu ya nyumba ya Bwana 1 kwa sababu watu wamevunja Agano langu, 2 wameasi dhidi ya sheria yangu. 1

2Israeli ananililia, 2 ‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’ 1

3Lakini Israeli amekataa lile lililo jema, 2 adui atamfuatia. 1

4Wanaweka wafalme bila idhini yangu, 2 wamechagua wakuu bila kibali changu. 1 Kwa fedha zao na dhahabu 2 wamejitengenezea sanamu kwa ajili 2 ya maangamizi yao wenyewe. 1

5Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama! 2 Hasira yangu inawaka dhidi yao. 1 Watakuwa najisi mpaka lini? 2

6Zimetoka katika Israeli! 1 Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu. 2 Atavunjwa vipande vipande, 2 yule ndama wa Samaria. 1

7“Wanapanda upepo 2 na kuvuna upepo wa kisulisuli. 1 Bua halina suke, 2 halitatoa unga. 1 Kama lingetoa nafaka, 2 wageni wangeila yote. 1

8Israeli amemezwa; 2 sasa yupo miongoni mwa mataifa 2 kama kitu kisicho na thamani. 1

9Kwa kuwa wamepanda kwenda Ashuru 2 kama punda-mwitu anayetangatanga peke yake. 1 Efraimu amejiuza mwenyewe 2 kwa wapenzi. 1

10Ingawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa, 2 sasa nitawakusanya pamoja. 1 Wataanza kudhoofika chini ya uonevu 2 wa mfalme mwenye nguvu. 1

11“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi 2 kwa ajili ya sadaka za dhambi, 1 hizi zimekuwa madhabahu 2 za kufanyia dhambi. 1

12Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi 2 kuhusu sheria yangu, 1 lakini wameziangalia 2 kama kitu cha kigeni. 1

13Wanatoa dhabihu nilizopewa mimi 2 nao wanakula hiyo nyama, 2 lakini Bwana hapendezwi nao. 1 Sasa ataukumbuka uovu wao 2 na kuadhibu dhambi zao: 2 Watarudi Misri. 1

14Israeli amemsahau Muumba wake 2 na kujenga majumba ya kifalme, 2 Yuda amejengea miji mingi ngome. 1 Lakini nitatuma moto kwenye miji yao 2 utakaoteketeza ngome zao.”

← Hosea 7Read In The App, Free →Hosea 9 →

Study Hosea 8

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314