Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 13

1Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka, 2 alikuwa ametukuzwa katika Israeli. 1 Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali 2 naye akafa. 1

2Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi; 2 wanajitengenezea sanamu 2 kutokana na fedha yao, 1 vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari, 2 vyote kazi ya fundi stadi. 1 Inasemekana kuhusu hawa watu, 2 “Hutoa dhabihu za binadamu 2 na kubusu sanamu za ndama.” 1

3Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, 2 kama umande wa alfajiri utowekao, 1 kama makapi yapeperushwayo 2 kutoka sakafu ya kupuria nafaka, 2 kama moshi utorokao kupitia dirishani. 1

4“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, 2 niliyewaleta ninyi toka Misri. 1 Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, 2 hakuna Mwokozi isipokuwa mimi. 1

5Niliwatunza huko jangwani, 2 katika nchi yenye joto liunguzalo. 1

6Nilipowalisha, walishiba, 2 waliposhiba, wakajivuna, 2 kisha wakanisahau mimi. 1

7Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, 2 kama chui nitawavizia kando ya njia. 1

8Kama dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, 2 nitawashambulia na kurarua vifua vyenu. 1 Kama simba nitawala; 2 mnyama pori atawararua vipande vipande. 1

9“Ee Israeli, umeangamizwa, 2 kwa sababu wewe u kinyume nami, 2 kinyume na msaidizi wako. 1

10Yuko wapi mfalme wako, 2 ili apate kukuokoa? 1 Wako wapi watawala wako katika miji yako yote 2 ambao ulisema kuwahusu, 2 ‘Nipe mfalme na wakuu’? 1

11Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme 2 na katika ghadhabu yangu nilimwondoa. 1

12Kosa la Efraimu limehifadhiwa, 2 dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu. 1

13Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia, 2 lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima; 1 wakati utakapowadia hatatoka 2 katika tumbo la mama yake. 1

14“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, 2 nitawakomboa kutoka mautini. 1 Yako wapi, ee mauti, mateso yako? 1 Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? 1 “Sitakuwa na huruma, 2

15hata ingawa Efraimu atastawi 2 miongoni mwa ndugu zake. 1 Upepo wa mashariki kutoka kwa Bwana utakuja, 2 ukivuma kutoka jangwani, 1 chemchemi yake haitatoa maji 2 na kisima chake kitakauka. 1 Ghala lake litatekwa 2 hazina zake zote. 1

16Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao, 2 kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao. 1 Wataanguka kwa upanga; 2 watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini, 2 wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”

← Hosea 12Read In The App, Free →Hosea 14 →

Study Hosea 13

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314