Proverbs 10
1Mithali za Solomoni: 1 Mwana mwenye hekima 2 huleta furaha kwa baba yake, 1 lakini mwana mpumbavu 2 huleta huzuni kwa mama yake. 1
2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, 2 lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 1
3Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, 2 lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 1
4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini 2 lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. 1
5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi 2 ni mwana mwenye hekima, 1 lakini yeye alalaye wakati wa mavuno 2 ni mwana mwenye kuaibisha. 1
6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, 2 lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 1
7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, 2 lakini jina la mwovu litaoza. 1
8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, 2 lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 1
9Mtu mwadilifu hutembea salama, 2 lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. 1
10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, 2 naye mpumbavu apayukaye huangamia. 1
11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, 2 lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 1
12Chuki huchochea faraka, 2 lakini upendo husitiri mabaya yote. 1
13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, 2 lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. 1
14Wenye hekima huhifadhi maarifa, 2 bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi. 1
15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, 2 bali ufukara ni maangamizi ya maskini. 1
16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, 2 lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. 1
17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, 2 lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. 1
18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, 2 na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 1
19Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, 2 lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. 1
20Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora, 2 bali moyo wa mwovu una thamani ndogo. 1
21Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, 2 lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu. 1
22Baraka ya Bwana hutajirisha, 2 wala haichanganyi huzuni. 1
23Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, 2 lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima. 1
24Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; 2 kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa. 1
25Tufani inapopita, waovu hutoweka, 2 lakini wenye haki husimama imara milele. 1
26Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, 2 ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. 1
27Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, 2 lakini miaka ya mwovu inafupishwa. 1
28Tarajio la mwenye haki ni furaha, 2 bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. 1
29Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, 2 lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya. 1
30Kamwe wenye haki hawataondolewa, 2 bali waovu hawatasalia katika nchi. 1
31Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, 2 bali ulimi wa upotovu utakatwa. 1
32Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, 2 bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.