Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 4

1Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu; 2 sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu. 1

2Ninawapa mafundisho ya maana, 2 kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. 1

3Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu, 2 ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu, 1

4baba alinifundisha akisema, 2 “Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote; 2 yashike maagizo yangu na wewe utaishi. 1

5Pata hekima, pata ufahamu; 2 usiyasahau maneno yangu wala usiyaache. 1

6Usimwache hekima naye atakuweka salama; 2 mpende, naye atakulinda. 1

7Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. 2 Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. 1

8Mstahi, naye atakukweza; 2 mkumbatie, naye atakuheshimu. 1

9Atakuvika shada la neema kichwani mwako 2 na kukupa taji ya utukufu.” 1

10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, 2 nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 1

11Ninakuongoza katika njia ya hekima 2 na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka. 1

12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa; 2 ukimbiapo, hutajikwaa. 1

13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; 2 mshike, maana yeye ni uzima wako. 1

14Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu 2 wala usitembee katika njia ya watu wabaya. 1

15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; 2 achana nayo, na uelekee njia yako. 1

16Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu; 2 wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu. 1

17Wanakula mkate wa uovu, 2 na kunywa mvinyo wa jeuri. 1

18Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, 2 ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu. 1

19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; 2 hawajui kinachowafanya wajikwae. 1

20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; 2 sikiliza kwa makini maneno yangu. 1

21Usiruhusu yaondoke machoni pako, 2 yahifadhi ndani ya moyo wako; 1

22kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata 2 na afya kwa mwili wote wa mwanadamu. 1

23Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, 2 maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 1

24Epusha kinywa chako na ukaidi; 2 weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako. 1

25Macho yako na yatazame mbele, 2 kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. 1

26Sawazisha mapito ya miguu yako 2 na njia zako zote ziwe zimethibitika. 1

27Usigeuke kulia wala kushoto; 2 epusha mguu wako na ubaya.

← Proverbs 3Read In The App, Free →Proverbs 5 →

Study Proverbs 4

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031