Proverbs 31
1Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha: 1
2“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, 2 ee mwana wa nadhiri zangu, + 31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu. 1
3Usitumie nguvu zako kwa wanawake, 2 uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme. 1
4“Ee Lemueli, haifai wafalme, 2 haifai wafalme kunywa mvinyo, 2 haifai watawala kutamani sana kileo, 1
5wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru 2 na kuwanyima haki zao wote walioonewa. 1
6Wape kileo wale wanaoangamia, 2 mvinyo wale walio na uchungu, 1
7Wanywe na kusahau umaskini wao 2 na wasikumbuke taabu yao tena. 1
8“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, 2 kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa. 1
9Sema na uamue kwa haki, 2 tetea haki za maskini na wahitaji.” 1 Maneno Ya Mwisho: Mke Mwenye Sifa Nzuri 1
10Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? 2 Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. + 31:10 Mithali 31:10-31 imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 1
11Mume wake anamwamini kikamilifu 2 wala hakosi kitu chochote cha thamani. 1
12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, 2 siku zote za maisha yake. 1
13Huchagua sufu na kitani 2 naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. 1
14Yeye ni kama meli za biashara 2 akileta chakula chake kutoka mbali. 1
15Yeye huamka kungali bado giza 2 huwapa jamaa yake chakula 2 na mafungu kwa watumishi wake wa kike. 1
16Huangalia shamba na kulinunua, 2 kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu. 1
17Hufanya kazi zake kwa nguvu, 2 mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake. 1
18Huona kwamba biashara yake ina faida, 2 wala taa yake haizimiki usiku. 1
19Huweka mikono yake kwenye pia, 2 navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi. 1
20Huwanyooshea maskini mikono yake 2 na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake. 1
21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, 2 kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto. 1
22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, 2 yeye huvaa kitani safi na urujuani. 1
23Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, 2 aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. 1
24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, 2 naye huwauzia wafanyabiashara mishipi. 1
25Amevikwa nguvu na heshima, 2 anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo. 1
26Huzungumza kwa hekima 2 na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake. 1
27Huangalia mambo ya nyumbani mwake 2 wala hali chakula cha uvivu. 1
28Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, 2 mumewe pia humsifu, akisema: 1
29“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, 2 lakini wewe umewapita wote.” 1
30Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, 2 bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa. 1
31Mpe thawabu anayostahili, 2 nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.