Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 23

1Uketipo kula chakula na mtawala, 2 angalia vyema kile kilicho mbele yako, 1

2na utie kisu kooni mwako 2 kama ukiwa mlafi. 1

3Usitamani vyakula vyake vitamu 2 kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. 1

4Usijitaabishe ili kuupata utajiri, 2 uwe na hekima kuonyesha kujizuia. 1

5Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, 2 huwa kama umepata mabawa ghafula, 2 ukaruka na kutoweka angani kama tai. 1

6Usile chakula cha mtu mchoyo, 2 usitamani vyakula vyake vitamu, 1

7kwa maana yeye ni aina ya mtu 2 ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama. 1 Anakuambia, “Kula na kunywa,” 2 lakini moyo wake hauko pamoja nawe. 1

8Utatapika kile kidogo ulichokula, 2 nawe utakuwa umepoteza bure 2 maneno yako ya kumsifu. 1

9Usizungumze na mpumbavu, 2 kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako. 1

10Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani 2 wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, 1

11kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, 2 atalichukua shauri lao dhidi yako. 1

12Elekeza moyo wako kwenye mafundisho 2 na masikio yako kwenye maneno ya maarifa. 1

13Usimnyime mtoto adhabu, 2 ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa. 1

14Mwadhibu kwa fimbo 2 na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini. + 23:14 Mautini maana yake ni Kuzimu. 1

15Mwanangu, kama moyo wako una hekima, 2 basi moyo wangu utafurahi, 1

16utu wangu wa ndani utafurahi, 2 wakati midomo yako 2 itakapozungumza lililo sawa. 1

17Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, 2 bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana. 1

18Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, 2 nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. 1

19Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, 2 weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa. 1

20Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, 2 au wale walao nyama kwa pupa, 1

21kwa maana walevi na walafi huwa maskini, 2 nako kusinzia huwavika matambara. 1

22Msikilize baba yako, aliyekuzaa, 2 wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee. 1

23Nunua kweli wala usiiuze, 2 pata hekima, adabu na ufahamu. 1

24Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa, 2 naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia. 1

25Baba yako na mama yako na wafurahi, 2 mama aliyekuzaa na ashangilie! 1

26Mwanangu, nipe moyo wako, 2 macho yako na yafuate njia zangu, 1

27kwa maana kahaba ni shimo refu 2 na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba. 1

28Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia, 2 naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume. 1

29Ni nani mwenye ole? 2 Ni nani mwenye huzuni? 1 Ni nani mwenye ugomvi? 2 Ni nani mwenye malalamiko? 1 Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? 2 Ni nani mwenye macho mekundu? 1

30Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, 2 hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa. 1

31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, 2 wakati unapometameta kwenye bilauri, 2 wakati ushukapo taratibu! 1

32Mwishowe huuma kama nyoka 2 na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. 1

33Macho yako yataona mambo mageni 2 na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka. 1

34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, 2 alalaye juu ya kamba ya merikebu. 1

35Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! 2 Wamenichapa, lakini sisikii! 1 Nitaamka lini 2 ili nikanywe tena?”

← Proverbs 22Read In The App, Free →Proverbs 24 →

Study Proverbs 23

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031