Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 6

1Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, 2 ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi 2 kwa ajili ya mwingine, 1

2kama umetegwa na ulichosema, 2 umenaswa kwa maneno ya kinywa chako, 1

3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, 2 kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: 1 Nenda ukajinyenyekeshe kwake; 2 msihi jirani yako! 1

4Usiruhusu usingizi machoni pako, 2 usiruhusu kope zako zisinzie. 1

5Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, 2 kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji. 1

6Ewe mvivu, mwendee mchwa; 2 zitafakari njia zake ukapate hekima! 1

7Kwa maana yeye hana msimamizi, 2 wala mwangalizi, au mtawala, 1

8lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi 2 na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 1

9Ewe mvivu, utalala hata lini? 2 Utaamka lini kutoka usingizi wako? 1

10Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, 2 bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: 1

11hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, 2 na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. 1

12Mtu mbaya sana na mlaghai, 2 ambaye huzungukazunguka 3 na maneno ya upotovu, 2

13ambaye anakonyeza kwa jicho lake, 2 anayetoa ishara kwa miguu yake 2 na kuashiria kwa vidole vyake, 2

14ambaye hupanga ubaya 3 kwa udanganyifu moyoni mwake: 2 daima huchochea fitina. 1

15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula; 2 ataangamizwa mara, pasipo msaada. 1

16Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, 2 naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: 3

17macho ya kiburi, 3 ulimi udanganyao, 3 mikono imwagayo damu isiyo na hatia, 3

18moyo uwazao mipango miovu, 3 miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, 3

19shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, 3 na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu. 1 Onyo Dhidi Ya Uasherati 1

20Mwanangu, zishike amri za baba yako, 2 wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 1

21Yafunge katika moyo wako daima, 2 yakaze kuizunguka shingo yako. 1

22Wakati utembeapo, yatakuongoza; 2 wakati ulalapo, yatakulinda; 2 wakati uamkapo, yatazungumza nawe. 1

23Kwa maana amri hizi ni taa, 2 mafundisho haya ni mwanga 2 na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, 1

24yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, 2 kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka. 1

25Moyo wako usitamani uzuri wake 2 wala macho yake yasikuteke, 1

26kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, 2 hata ukose kipande cha mkate, 2 naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa. 1

27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake 2 bila nguo zake kuungua? 1

28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka 2 bila miguu yake kuungua? 1

29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; 2 hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa. 1

30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba 2 kukidhi njaa yake wakati ana njaa. 1

31Pamoja na hayo, kama akikamatwa, 2 lazima alipe mara saba, 2 ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake. 1

32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; 2 yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe. 1

33Mapigo na aibu ni fungu lake 2 na aibu yake haitafutika kamwe; 1

34kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, 2 naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi. 1

35Hatakubali fidia yoyote; 2 atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.

← Proverbs 5Read In The App, Free →Proverbs 7 →

Study Proverbs 6

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031