Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 28

1Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, 2 bali wenye haki ni wajasiri kama simba. 1

2Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, 2 bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. 1

3Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi 2 ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao. 1

4Wale waiachao sheria huwasifu waovu, 2 bali wale waishikao sheria huwapinga. 1

5Watu wabaya hawaelewi haki, 2 bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu. 1

6Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama 2 kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu. 1

7Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, 2 bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. 1

8Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno 2 hukusanya kwa ajili ya mwingine, 2 ambaye atawahurumia maskini. 1

9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, 2 hata maombi yake ni chukizo. 1

10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, 2 ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, 2 bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. 1

11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, 2 bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 1

12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, 2 bali waovu watawalapo, watu hujificha. 1

13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, 2 bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 1

14Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana, 2 bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu 2 huangukia kwenye taabu. 1

15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, 2 ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. 1

16Mtawala dhalimu hana akili, 2 bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu 2 atafurahia maisha marefu. 1

17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua 2 atakuwa mtoro mpaka kufa; 2 mtu yeyote na asimsaidie. 1

18Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama 2 hulindwa salama, 1 bali yeye ambaye njia zake ni potovu 2 ataanguka ghafula. 1

19Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, 2 bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha. 1

20Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, 2 bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka 2 hataacha kuadhibiwa. 1

21Kuonyesha upendeleo si vizuri, 2 hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate. 1

22Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, 2 naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. 1

23Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi, 2 kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili. 1

24Yeye amwibiaye babaye au mamaye 2 na kusema, “Si kosa,” 2 yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. 1

25Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, 2 bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa. 1

26Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, 2 bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. 1

27Yeye ampaye maskini 2 hatapungukiwa na kitu chochote, 1 bali yeye awafumbiaye maskini macho 2 hupata laana nyingi. 1

28Wakati waovu watawalapo, 2 watu huenda mafichoni, 1 bali waovu wanapoangamia, 2 wenye haki hufanikiwa.

← Proverbs 27Read In The App, Free →Proverbs 29 →

Study Proverbs 28

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031