Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 19

1Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, 2 kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. 1

2Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, 2 wala kufanya haraka na kuikosa njia. 1

3Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake 2 hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana. 1

4Mali huleta marafiki wengi, 2 bali rafiki wa mtu maskini humwacha. 1

5Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, 2 naye amwagaye uongo hataachwa huru. 1

6Wengi hujipendekeza kwa mtawala 2 na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. 1

7Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: 2 Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani! 1 Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, 2 hawapatikani popote. 1

8Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, 2 yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. 1

9Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, 2 naye amwagaye uongo ataangamia. 1

10Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, 2 itakuwa vibaya kiasi gani 2 kwa mtumwa kuwatawala wakuu. 1

11Hekima ya mtu humpa uvumilivu, 2 ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. 1

12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, 2 bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi. 1

13Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, 2 naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha. 1

14Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, 2 bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana. 1

15Uvivu huleta usingizi mzito, 2 naye mtu mzembe huona njaa. 1

16Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, 2 bali yeye anayezidharau njia zake atakufa. 1

17Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, 2 naye atamtuza kwa aliyotenda. 1

18Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, 2 usiwe mshirika katika mauti yake. 1

19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake, 2 kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena. 1

20Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, 2 nawe mwishoni utakuwa na hekima. 1

21Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, 2 lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama. 1

22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, 2 afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. 1

23Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima, 2 kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, 2 bila kuguswa na shida. 1

24Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, 2 lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake! 1

25Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara, 2 mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa. 1

26Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake 2 ni mwana aletaye aibu na fedheha. 1

27Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, 2 utatangatanga mbali na maneno ya maarifa. 1

28Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu 2 na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi. 1

29Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka 2 na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.

← Proverbs 18Read In The App, Free →Proverbs 20 →

Study Proverbs 19

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031