Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 14

1Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, 2 bali mpumbavu huibomoa nyumba yake 2 kwa mikono yake mwenyewe. 1

2Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, 2 bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 1

3Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, 2 bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. 1

4Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu, 2 bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi. 1

5Shahidi mwaminifu hadanganyi, 2 bali shahidi wa uongo humimina uongo. 1

6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, 2 bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. 1

7Kaa mbali na mtu mpumbavu, 2 kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. 1

8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, 2 bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. 1

9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, 2 bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu. 1

10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, 2 wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake. 1

11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, 2 bali hema la mnyofu litastawi. 1

12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, 2 bali mwisho wake huelekeza mautini. 1

13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, 2 nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. 1

14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, 2 naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake. 1

15Mtu mjinga huamini kila kitu, 2 bali mwenye busara hufikiria hatua zake. 1

16Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya, 2 bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. 1

17Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu, 2 naye mtu wa hila huchukiwa. 1

18Mjinga hurithi upumbavu, 2 bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. 1

19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, 2 nao waovu kwenye malango ya wenye haki. 1

20Maskini huepukwa hata na majirani zao, 2 bali matajiri wana marafiki wengi. 1

21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, 2 bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. 1

22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? 2 Bali wale wanaopanga kilicho chema 2 hupata upendo na uaminifu. 1

23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, 2 bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. 1

24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, 2 bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu. 1

25Shahidi wa kweli huokoa maisha, 2 bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu. 1

26Yeye amchaye Bwana ana ngome salama, 2 na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. 1

27Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, 2 ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. 1

28Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, 2 bali pasipo watu mkuu huangamia. 1

29Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, 2 bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu. 1

30Moyo wenye amani huupa mwili uzima, 2 bali wivu huozesha mifupa. 1

31Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, 2 bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. 1

32Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, 2 bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. 1

33Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu 2 bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu. 1

34Haki huinua taifa, 2 bali dhambi ni aibu kwa watu wote. 1

35Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, 2 bali ghadhabu yake humwangukia 2 mtumishi mwenye kuaibisha.

← Proverbs 13Read In The App, Free →Proverbs 15 →

Study Proverbs 14

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031