Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 20

1Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; 2 yeyote apotoshwaye navyo hana hekima. 1

2Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; 2 yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 1

3Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, 2 bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. 1

4Mvivu halimi kwa majira; 2 kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama 2 lakini hapati chochote. 1

5Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, 2 lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. 1

6Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, 2 bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? 1

7Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, 2 wamebarikiwa watoto wake baada yake. 1

8Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu, 2 hupepeta ubaya wote kwa macho yake. 1

9Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; 2 mimi ni safi na sina dhambi?” 1

10Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, 2 Bwana huchukia vyote viwili. 1

11Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, 2 kama tabia yake ni safi na adili. 1

12Masikio yasikiayo na macho yaonayo, 2 Bwana ndiye alivifanya vyote viwili. 1

13Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, 2 uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. 1

14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi, 2 kisha huondoka akijisifia ununuzi wake. 1

15Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi, 2 lakini midomo inenayo maarifa 2 ni kito cha thamani kilicho adimu. 1

16Chukua vazi la yule awekaye dhamana 2 kwa ajili ya mgeni; 1 lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo 2 kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 1

17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu, 2 bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe. 1

18Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, 2 ukipigana vita, tafuta maelekezo. 1

19Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika, 2 kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi. 1

20Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, 2 taa yake itazimwa katika giza nene. 1

21Urithi upatikanao haraka mwanzoni, 2 hautabarikiwa mwishoni. 1

22Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” 2 Mngojee Bwana, naye atakuokoa. 1

23Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, 2 nazo mizani zisizo halali hazimpendezi. 1

24Hatua za mtu huongozwa na Bwana. 2 Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe? 1

25Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka 2 na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake. 1

26Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu, 2 hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao. 1

27Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu, 2 huchunguza utu wake wa ndani. 1

28Upendo na uaminifu humweka mfalme salama, 2 kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama. 1

29Utukufu wa vijana ni nguvu zao, 2 mvi ni fahari ya uzee. 1

30Mapigo na majeraha huusafisha ubaya, 2 nayo michapo hutakasa utu wa ndani.

← Proverbs 19Read In The App, Free →Proverbs 21 →

Study Proverbs 20

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031