Proverbs 13
1Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye, 2 bali mwenye dharau hasikilizi maonyo. 1
2Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema, 2 bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri. 1
3Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake, 2 bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia. 1
4Mvivu hutamani sana na hapati kitu, 2 bali nafsi ya mwenye bidii 2 hutoshelezwa kikamilifu. 1
5Mwenye haki huchukia uongo, 2 bali waovu huleta aibu na fedheha. 1
6Haki humlinda mtu mwadilifu, 2 bali uovu humwangusha mwenye dhambi. 1
7Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; 1 mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi. 1
8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, 2 bali mtu maskini hasikii kitisho. 1
9Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana, 2 bali taa ya mwovu itazimwa. 1
10Kiburi huzalisha magomvi tu, 2 bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri. 1
11Fedha isiyo ya halali hupungua, 2 bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. 1
12Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, 2 bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima. 1
13Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi, 2 bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo. 1
14Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima, 2 ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. 1
15Ufahamu mzuri hupata upendeleo, 2 bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu. 1
16Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, 2 bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake. 1
17Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu, 2 bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji. 1
18Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, 2 bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. 1
19Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, 2 bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya. 1
20Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima, 2 bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara. 1
21Balaa humwandama mtenda dhambi, 2 bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki. 1
22Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, 2 bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa 2 kwa ajili ya wenye haki. 1
23Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, 2 bali dhuluma hukifutilia mbali. 1
24Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, 2 bali yeye ampendaye 2 huwa mwangalifu kumwadibisha. 1
25Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake, 2 bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.