Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 25

1Hizi ni mithali zaidi za Solomoni, zilizonakiliwa na watu wa Hezekia mfalme wa Yuda: 1

2Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, 2 bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. 1

3Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, 2 ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. 1

4Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, 2 nako ndani yake kutatokea chombo 2 cha mfua fedha. 1

5Ondoa waovu mbele ya mfalme, 2 nacho kiti chake cha enzi 2 kitaimarishwa kwa njia ya haki. 1

6Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, 2 wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; 1

7ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” 2 kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. 1 Kile ulichokiona kwa macho yako 2

8usiharakishe kukipeleka mahakamani, 1 maana utafanya nini mwishoni 2 kama jirani yako atakuaibisha? 1

9Kama ukifanya shauri na jirani yako, 2 usisaliti siri ya mtu mwingine, 1

10ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha 2 na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. 1

11Neno lisemwalo kwa wakati ufaao 2 ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu 2 yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. 1

12Kama vile kipuli cha dhahabu 2 au pambo la dhahabu safi, 1 ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima 2 kwa sikio lisikilizalo. 1

13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno 2 ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, 2 huburudisha roho za bwana zake. 1

14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua 2 ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. 1

15Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, 2 nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa. 1

16Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, 2 ukila zaidi, utatapika. 1

17Ingiza mguu wako nyumbani kwa jirani yako mara chache, 2 ukizidisha, atakukinai na atakuchukia. 1

18Kama vile rungu au upanga au mshale mkali 2 ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake. 1

19Kama vile jino bovu au mguu uliolemaa, 2 ndivyo ilivyo kumtegemea mtu asiye mwaminifu wakati wa shida. 1

20Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi, 2 au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi, 2 ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito. 1

21Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale; 2 kama ana kiu, mpe maji anywe. 1

22Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, 2 naye Bwana atakupa thawabu. 1

23Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua, 2 ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira. 1

24Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, 2 kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. 1

25Kama vile maji baridi kwa nafsi iliyochoka 2 ndivyo zilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali. 1

26Kama vile chemchemi iliyotibuliwa matope au 2 kisima kilichotiwa taka 1 ndivyo alivyo mtu mwenye haki 2 akishiriki na waovu. 1

27Si vyema kula asali nyingi sana, 2 wala si heshima 2 kujitafutia heshima yako mwenyewe. 1

28Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka 2 ndivyo alivyo mtu 2 ambaye hawezi kujitawala mwenyewe.

← Proverbs 24Read In The App, Free →Proverbs 26 →

Study Proverbs 25

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031