Proverbs 18
1Mtu ajitengaye na wengine 2 hufuata matakwa yake mwenyewe; 2 hupiga vita kila shauri jema. 1
2Mpumbavu hafurahii ufahamu, 2 bali hufurahia kutangaza 2 maoni yake mwenyewe. 1
3Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, 2 pamoja na aibu huja lawama. 1
4Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, 2 bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika. 1
5Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, 2 au kumnyima haki asiye na hatia. 1
6Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi 2 na kinywa chake hualika kipigo. 1
7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake 2 na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake. 1
8Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; 2 huingia sehemu za ndani sana za mtu. 1
9Mtu aliye mlegevu katika kazi yake 2 ni ndugu na yule anayeharibu. 1
10Jina la Bwana ni ngome imara, 2 wenye haki huikimbilia na kuwa salama. 1
11Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, 2 wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa. 1
12Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, 2 bali unyenyekevu hutangulia heshima. 1
13Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, 2 huo ni upumbavu wake na aibu yake. 1
14Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa 2 bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili? 1
15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, 2 masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa. 1
16Zawadi humfungulia njia mtoaji, 2 nayo humleta mbele ya wakuu. 1
17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi, 2 hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali. 1
18Kupiga kura hukomesha mashindano 2 na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana. 1
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika 2 kuliko mji uliozungushiwa ngome, 1 nayo mabishano ni kama malango 2 ya ngome yenye makomeo. 1
20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, 2 atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake. 1
21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, 2 nao waupendao watakula matunda yake. 1
22Apataye mke apata kitu chema 2 naye ajipatia kibali kwa Bwana. 1
23Mtu maskini huomba kuhurumiwa 2 bali tajiri hujibu kwa ukali. 1
24Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, 2 bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.