Proverbs 30
1Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia: 1 Huyu mtu alimwambia Ithieli, 2 naam, kwa Ithieli na kwa Ukali: 1
2“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; 2 sina ufahamu wa kibinadamu. 1
3Sijajifunza hekima, 2 wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. 1
4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? 2 Ni nani ameshakusanya upepo 2 kwenye vitanga vya mikono yake? 1 Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? 2 Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? 1 Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? 2 Niambie kama unajua! 1
5“Kila neno la Mungu ni kamilifu; 2 yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. 1
6Usiongeze kwenye maneno yake, 2 ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo. 1
7“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana; 2 usininyime kabla sijafa: 1
8Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; 2 usinipe umaskini wala utajiri, 2 bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. 1
9Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana 2 na kusema, ‘ Bwana ni nani?’ 1 Au nisije nikawa maskini nikaiba, 2 nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu. 1
10“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake, 2 asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo. 1
11“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao 2 na wala hawawabariki mama zao; 1
12wale ambao ni safi machoni pao wenyewe 2 kumbe hawakuoshwa uchafu wao; 1
13wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, 2 ambao kutazama kwao ni kwa dharau; 1
14wale ambao meno yao ni panga 2 na ambao mataya yao yamewekwa visu 1 kuwaangamiza maskini katika nchi, 2 na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu. 1
15“Mruba anao binti wawili waliao, 2 ‘Nipe! Nipe!’ 1 “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, 2 naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: 1
16Ni kaburi, tumbo lisilozaa, 2 nchi isiyoshiba maji kamwe, 2 na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ 1
17“Jicho lile limdhihakilo baba, 2 lile linalodharau kumtii mama, 1 litangʼolewa na kunguru wa bondeni, 2 litaliwa na tai. 1
18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, 2 naam, vinne nisivyovielewa: 1
19Ni mwendo wa tai katika anga, 2 mwendo wa nyoka juu ya mwamba, 1 mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, 2 nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. 1
20“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi, 2 hula akapangusa kinywa chake na kusema, 2 ‘Sikufanya chochote kibaya.’ 1
21“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, 2 naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia: 1
22Mtumwa awapo mfalme, 2 mpumbavu ashibapo chakula, 1
23mwanamke asiyependwa aolewapo, 2 naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake. 1
24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, 2 lakini vina akili nyingi sana: 1
25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, 2 hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi. 1
26Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo 2 hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. 1
27Nzige hawana mfalme, 2 hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi. 1
28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, 2 hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme. 1
29“Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, 2 naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha: 1
30simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, 2 asiyerudi nyuma kwa chochote; 1
31jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, 2 naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka. 1
32“Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe, 2 au kama umepanga mabaya, 2 basi funika mdomo wako na mkono wako. 1
33Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi, 2 na pia kule kufinya pua hutoa damu, 2 kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.”