Proverbs 22
1Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi, 2 kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu. 1
2Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: 2 Bwana ni Muumba wao wote. 1
3Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, 2 bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa. 1
4Unyenyekevu na kumcha Bwana 2 huleta utajiri, heshima na uzima. 1
5Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, 2 bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. 1
6Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, 2 naye hataiacha hata akiwa mzee. 1
7Matajiri huwatawala maskini 2 naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. 1
8Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, 2 nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. 1
9Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa 2 kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini. 1
10Mfukuze mwenye dhihaka, 2 na mvutano utatoweka; 2 ugomvi na matukano vitakoma. 1
11Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, 2 mfalme atakuwa rafiki yake. 1
12Macho ya Bwana hulinda maarifa, 2 bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. 1
13Mvivu husema, “Yuko simba nje!” 2 au, “Nitauawa katika mitaa!” 1
14Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; 2 yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana 2 atatumbukia ndani yake. 1
15Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, 2 bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. 1
16Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali, 2 naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini. 1 Misemo Ya Wenye Hekima 1
17Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, 2 elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, 1
18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako 2 na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako. 1
19Ili tumaini lako liwe katika Bwana, 2 hata wewe, ninakufundisha leo. 1
20Je, sijakuandikia misemo thelathini, 2 misemo ya mashauri na maarifa, 1
21kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, 2 ili uweze kutoa majibu sahihi 2 kwake yeye aliyekutuma? 1
22Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, 2 wala kumdhulumu mhitaji mahakamani, 1
23kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao 2 naye atawateka wao waliowateka. 1
24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, 2 usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika, 1
25la sivyo utajifunza njia zake 2 na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego. 1
26Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani, 2 au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni. 1
27Kama ukikosa njia ya kulipa, 2 kitanda chako 2 kitachukuliwa ukiwa umekilalia. 1
28Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani 2 lililowekwa na baba zako. 1
29Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? 2 Atahudumu mbele ya wafalme; 2 hatahudumu mbele ya watu duni.