Proverbs 5
1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, 2 sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, 1
2ili uweze kutunza busara 2 na midomo yako ihifadhi maarifa. 1
3Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba 2 hudondoza asali, 1 na maneno ya kinywa chake 2 ni laini kuliko mafuta; 1
4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, 2 mkali kama upanga ukatao kuwili. 1
5Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; 2 hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. + 5:5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 1
6Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; 2 njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. 1
7Sasa basi wanangu, nisikilizeni; 2 msiache ninalowaambia. 1
8Njia zenu ziwe mbali naye, 2 msiende karibu na mlango wa nyumba yake, 1
9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine 2 na miaka yako kwa aliye mkatili, 1
10wageni wasije wakasherehekea utajiri wako 2 na jitihada yako ikatajirisha 2 nyumba ya mwanaume mwingine. 1
11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, 2 wakati nyama na mwili wako vimechakaa. 1
12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! 2 Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! 1
13Sikuwatii walimu wangu 2 wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. 1
14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa 2 katikati ya kusanyiko lote.” 1
15Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, 2 maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe. 1
16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji 2 na vijito vyako vya maji viwanjani? 1
17Na viwe vyako mwenyewe, 2 kamwe visishirikishwe wageni. 1
18Chemchemi yako na ibarikiwe 2 na umfurahie mke wa ujana wako. 1
19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: 2 matiti yake na yakutosheleze siku zote, 2 nawe utekwe daima na upendo wake. 1
20Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? 2 Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine? 1
21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, 2 naye huyapima mapito yake yote. 1
22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; 2 kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu. 1
23Atakufa kwa kukosa nidhamu, 2 akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.