Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 12

1Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, 2 bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu. 1

2Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana, 2 bali Bwana humhukumu mwenye hila. 1

3Mtu hathibitiki kutokana na uovu, 2 bali mwenye haki hataondolewa. 1

4Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, 2 bali aaibishaye ni kama uozo 2 katika mifupa ya mumewe. 1

5Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, 2 bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu. 1

6Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, 2 bali maneno ya waadilifu huwaokoa. 1

7Watu waovu huondolewa na kutoweka, 2 bali nyumba ya mwenye haki husimama imara. 1

8Mtu husifiwa kulingana na hekima yake, 2 bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa. 1

9Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi, 2 kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula. 1

10Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, 2 bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. 1

11Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, 2 bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili. 1

12Waovu hutamani mateka ya watu wabaya, 2 bali shina la mwenye haki hustawi. 1

13Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, 2 bali mwenye haki huepuka taabu. 1

14Kutokana na tunda la midomo yake 2 mtu hujazwa na mambo mema, 2 hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza. 1

15Njia ya mpumbavu huonekana sawa 2 machoni pake mwenyewe, 2 bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri. 1

16Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, 2 bali mtu wa busara hupuuza matukano. 1

17Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika, 2 bali shahidi wa uongo husema uongo. 1

18Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, 2 bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji. 1

19Midomo isemayo kweli hudumu milele, 2 bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu. 1

20Upo udanganyifu katika mioyo 2 ya wale ambao hupanga mabaya, 2 bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani. 1

21Hakuna dhara linalompata mwenye haki, 2 bali waovu wana taabu nyingi. 1

22Bwana anachukia sana midomo idanganyayo, 2 bali hufurahia watu ambao ni wa kweli. 1

23Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, 2 bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu. 1

24Mikono yenye bidii itatawala, 2 bali uvivu huishia katika kazi za utumwa. 1

25Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, 2 bali neno la huruma humfurahisha. 1

26Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, 2 bali njia ya waovu huwapotosha. 1

27Mtu mvivu haoki mawindo yake, 2 bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani. 1

28Katika njia ya haki kuna uzima; 2 katika mapito hayo kuna maisha ya milele.

← Proverbs 11Read In The App, Free →Proverbs 13 →

Study Proverbs 12

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031