Proverbs 26
1Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, 2 ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu. 1
2Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake 2 au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, 2 ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu. 1
3Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, 2 nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu! 1
4Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, 2 ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye. 1
5Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, 2 ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. 1
6Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, 2 ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. 1
7Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia 2 ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. 1
8Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, 2 ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima. 1
9Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi 2 ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu. 1
10Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, 2 ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani. 1
11Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, 2 ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. 1
12Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima 2 machoni pake mwenyewe? 2 Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. 1
13Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, 2 simba mkali anazunguka mitaa!” 1
14Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, 2 ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. 1
15Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, 2 naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. 1
16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, 2 kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. 1
17Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, 2 ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. 1
18Kama mtu mwendawazimu 2 atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha, 1
19ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, 2 “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” 1
20Bila kuni moto huzimika; 2 pasipo uchongezi ugomvi humalizika. 1
21Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, 2 ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. 1
22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; 2 huingia sehemu za ndani sana za mtu. 1
23Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo 2 ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya. 1
24Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, 2 lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. 1
25Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, 2 kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. 1
26Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, 2 lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. 1
27Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, 2 kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia. 1
28Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, 2 nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.