Proverbs 24
1Usiwaonee wivu watu waovu, 2 usitamani ushirika nao; 1
2kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, 2 nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara. 1
3Kwa hekima nyumba hujengwa, 2 nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa 1
4kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa 2 vitu vya thamani na vya kupendeza. 1
5Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, 2 naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, 1
6kwa kufanya vita unahitaji uongozi 2 na kwa ushindi washauri wengi. 1
7Hekima i juu mno kwa mpumbavu, 2 katika kusanyiko langoni 2 hana lolote la kusema. 1
8Yeye apangaye mabaya 2 atajulikana kama mtu wa hila. 1
9Mipango ya upumbavu ni dhambi, 2 watu huchukizwa na mwenye dhihaka. 1
10Ukikata tamaa wakati wa taabu, 2 jinsi gani nguvu zako ni kidogo! 1
11Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; 2 wazuie wote wanaojikokota 2 kuelekea machinjoni. 1
12Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” 2 je, yule apimaye mioyo halitambui hili? 1 Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? 2 Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda? 1
13Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; 2 asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. 1
14Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, 2 kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, 2 nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. 1
15Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia 2 makao ya mwenye haki, 2 wala usiyavamie makazi yake, 1
16Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, 2 lakini waovu huangushwa chini na maafa. 1
17Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; 2 wakati ajikwaapo, 2 usiruhusu moyo wako ushangilie. 1
18Bwana asije akaona na kuchukia 2 akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. 1
19Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya 2 wala usiwaonee wivu waovu, 1
20kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, 2 nayo taa ya waovu itazimwa. 1
21Mwanangu, mche Bwana na mfalme, 2 wala usijiunge na waasi, 1
22kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, 2 naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta? 1 Misemo Zaidi Ya Wenye Hekima
23Hii pia ni misemo ya wenye hekima: 1 Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema: 1
24Yeyote amwambiaye mwenye hatia, 2 “Wewe huna hatia,” 1 Kabila zitamlaani 2 na mataifa yatamkana. 1
25Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, 2 nazo baraka tele zitawajilia juu yao. 1
26Jawabu la uaminifu 2 ni kama busu la midomoni. 1
27Maliza kazi zako za nje, 2 nawe uweke mashamba yako tayari, 2 baada ya hayo, jenga nyumba yako. 1
28Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, 2 au kutumia midomo yako kudanganya. 1
29Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; 2 nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.” 1
30Nilipita karibu na shamba la mvivu, 2 karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, 1
31miiba ilikuwa imeota kila mahali, 2 ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na 2 ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka. 1
32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, 2 nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona: 1
33Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, 2 bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: 1
34hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, 2 na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.