Proverbs 27
1Usijisifu kwa ajili ya kesho, 2 kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. 1
2Mwache mwingine akusifu, 2 wala si kinywa chako mwenyewe; 1 mtu mwingine afanye hivyo 2 na si midomo yako mwenyewe. 1
3Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, 2 lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili. 1
4Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, 2 lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu? 1
5Afadhali karipio la wazi 2 kuliko upendo uliofichika. 1
6Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, 2 bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. 1
7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, 2 bali kwa mwenye njaa 2 hata kile kilicho kichungu 2 kwake ni kitamu. 1
8Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, 2 ndivyo alivyo mtu atangatangaye 2 mbali na nyumbani mwake. 1
9Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, 2 nao uzuri wa rafiki huchipuka 2 kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu. 1
10Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, 2 tena usiende nyumbani mwa ndugu yako 2 wakati umepatwa na maafa. 1 Bora jirani wa karibu 2 kuliko ndugu aliye mbali. 1
11Mwanangu, uwe na hekima, 2 nawe ulete furaha moyoni mwangu, 1 ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote 2 anitendaye kwa dharau. 1
12Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, 2 bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa. 1
13Chukua vazi la yule awekaye dhamana 2 kwa ajili ya mgeni; 1 lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo 2 kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 1
14Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu 2 asubuhi na mapema, 2 itahesabiwa kama ni laana. 1
15Mke mgomvi ni kama 2 matone yasiyokoma ya siku ya mvua. 1
16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo 2 au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. 1
17Kama vile chuma kinoavyo chuma, 2 ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. 1
18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, 2 naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. 1
19Kama uso uonekanavyo kwenye maji, 2 ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo. 1
20Kuzimu na Uharibifu havishibi 2 kadhalika macho ya mwanadamu. 1
21Kalibu ni kwa ajili ya fedha 2 na tanuru kwa ajili ya dhahabu, 2 bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo. 1
22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, 2 ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, 2 hutauondoa upumbavu wake. 1
23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako 2 ya kondoo na mbuzi, 2 angalia kwa bidii ngʼombe zako. 1
24Kwa kuwa utajiri haudumu milele, 2 nayo taji haidumu vizazi vyote. 1
25Wakati majani makavu yameondolewa 2 na mapya yamechipua, 2 nayo majani toka milimani yamekusanywa, 1
26wana-kondoo watakupatia mavazi 2 na mbuzi thamani ya shamba. 1
27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi 2 kukulisha wewe na jamaa yako, 2 na kuwalisha watumishi wako wa kike.