Proverbs 8
1Je, hekima haitani? 2 Je, ufahamu hapazi sauti? 1
2Juu ya miinuko karibu na njia, 2 penye njia panda, ndipo asimamapo; 1
3kando ya malango yaelekeayo mjini, 2 kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: 1
4“Ni ninyi wanaume, ninaowaita; 2 ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. 1
5Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; 2 ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu. 1
6Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; 2 ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa. 1
7Kinywa changu husema lililo kweli, 2 kwa maana midomo yangu huchukia uovu. 1
8Maneno yote ya kinywa changu ni haki; 2 hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi. 1
9Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi; 2 hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. 1
10Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, 2 maarifa badala ya dhahabu safi, 1
11kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani 2 na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. 1
12“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; 2 ninamiliki maarifa na busara. 1
13Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; 2 ninachukia kiburi na majivuno, 2 tabia mbaya na mazungumzo potovu. 1
14Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; 2 nina ufahamu na nina nguvu. 1
15Kwa msaada wangu wafalme hutawala 2 na watawala hutunga sheria zilizo za haki, 1
16kwa msaada wangu wakuu hutawala, 2 na wenye vyeo wote watawalao dunia. 1
17Nawapenda wale wanipendao, 2 na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. 1
18Utajiri na heshima viko kwangu, 2 utajiri udumuo na mafanikio. 1
19Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi; 2 kile nitoacho hupita fedha iliyo bora. 1
20Natembea katika njia ya unyofu 2 katika mapito ya haki, 1
21nawapa utajiri wale wanipendao 2 na kuzijaza hazina zao. 1
22“ Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, 2 kabla ya matendo yake ya zamani; 1
23niliteuliwa tangu milele, 2 tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. 1
24Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa, 2 wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji; 1
25kabla milima haijawekwa mahali pake, 2 kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa, 1
26kabla hajaumba dunia wala mashamba yake 2 au vumbi lolote la dunia. 1
27Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake, 2 wakati alichora mstari wa upeo wa macho 3 juu ya uso wa kilindi, 1
28wakati aliweka mawingu juu 2 na kuziweka imara chemchemi za bahari, 1
29wakati aliiwekea bahari mpaka wake 2 ili maji yasivunje agizo lake, 1 na wakati aliweka misingi ya dunia. 2
30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake. 1 Nilijazwa na furaha siku baada ya siku, 2 nikifurahi daima mbele zake, 1
31nikifurahi katika dunia yake yote 2 nami nikiwafurahia wanadamu. 1
32“Basi sasa wanangu, nisikilizeni; 2 heri wale wanaozishika njia zangu. 1
33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima; 2 msiyapuuze. 1
34Heri mtu yule anisikilizaye mimi, 2 akisubiri siku zote malangoni mwangu, 2 akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu. 1
35Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima 2 na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana. 1
36Lakini yeyote ashindwaye kunipata 2 hujiumiza mwenyewe; 2 na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.”