Proverbs 2
1Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu 2 na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, 1
2kutega sikio lako kwenye hekima 2 na kuweka moyo wako katika ufahamu, 1
3na kama ukiita busara 2 na kuita kwa sauti ufahamu, 1
4na kama utaitafuta kama fedha 2 na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, 1
5ndipo utakapoelewa kumcha Bwana 2 na kupata maarifa ya Mungu. 1
6Kwa maana Bwana hutoa hekima, 2 na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. 1
7Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, 2 yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, 1
8kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki 2 na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. 1
9Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki 2 na sawa: yaani kila njia nzuri. 1
10Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, 2 nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako. 1
11Busara itakuhifadhi 2 na ufahamu utakulinda. 1
12Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, 2 kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, 1
13wale waachao mapito yaliyonyooka 2 wakatembea katika njia za giza, 1
14wale wapendao kutenda mabaya 2 na kufurahia upotovu wa ubaya, 1
15ambao mapito yao yamepotoka 2 na ambao ni wapotovu katika njia zao. 1
16Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, 2 kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno 2 ya kushawishi kutenda ubaya, 1
17aliyemwacha mwenzi wa ujana wake 2 na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu. 1
18Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo 2 na mapito yake kwenye roho za waliokufa. 1
19Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, 2 au kufikia mapito ya uzima. 1
20Hivyo utatembea katika njia za watu wema 2 na kushikamana na mapito ya wenye haki. 1
21Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, 2 nao wasio na lawama watabakia ndani yake. 1
22Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, 2 nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.