Proverbs 15
1Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, 2 bali neno liumizalo huchochea hasira. 1
2Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, 2 bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. 1
3Macho ya Bwana yako kila mahali, 2 yakiwaangalia waovu na wema. 1
4Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, 2 bali ulimi udanganyao huponda roho. 1
5Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, 2 bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara. 1
6Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, 2 bali mapato ya waovu huwaletea taabu. 1
7Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, 2 bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. 1
8Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, 2 bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. 1
9Bwana huchukia sana njia ya waovu, 2 bali huwapenda wale wafuatao haki. 1
10Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; 2 yeye achukiaye maonyo atakufa. 1
11Mauti + 15:11 Yaani Sheol, maana yake ni Kuzimu. na Uharibifu + 15:11 Kwa Kiebrania ni Abadon. viko wazi mbele za Bwana: 2 je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! 1
12Mwenye mzaha huchukia maonyo; 2 hatataka shauri kwa mwenye hekima. 1
13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, 2 bali maumivu ya moyoni huponda roho. 1
14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, 2 bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu. 1
15Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, 2 bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu. 1
16Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, 2 kuliko mali nyingi pamoja na ghasia. 1
17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo 2 kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. 1
18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, 2 bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi. 1
19Njia ya mvivu imezibwa na miiba, 2 bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu. 1
20Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, 2 bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. 1
21Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, 2 bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka. 1
22Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri, 2 bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa. 1
23Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa: 2 je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake! 1
24Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima 2 kumwepusha asiende chini kaburini. 1
25Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, 2 bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe. 1
26Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, 2 bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. 1
27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, 2 bali yeye achukiaye rushwa ataishi. 1
28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, 2 bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. 1
29Bwana yuko mbali na waovu, 2 bali husikia maombi ya wenye haki. 1
30Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, 2 nazo habari njema huipa mifupa afya. 1
31Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima 2 atakuwa miongoni mwa wenye hekima. 1
32Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe, 2 bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu. 1
33Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima, 2 nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.