Proverbs 9
1Hekima amejenga nyumba yake; 2 amechonga nguzo zake saba. 1
2Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; 2 pia ameandaa meza yake. 1
3Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita 2 kutoka mahali pa juu sana pa mji. 1
4Anawaambia wale wasio na akili, 2 “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! 1
5Njooni, mle chakula changu 2 na mnywe divai niliyoichanganya. 1
6Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; 2 tembeeni katika njia ya ufahamu. 1
7“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha 2 hukaribisha matukano; 1 yeyote anayekemea mtu mwovu 2 hupatwa na matusi. 1
8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; 2 mkemee mwenye hekima naye atakupenda. 1
9Mfundishe mtu mwenye hekima 2 naye atakuwa na hekima zaidi; 1 mfundishe mtu mwadilifu 2 naye atazidi kufundishika. 1
10“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, 2 na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. 1
11Kwa maana kwa msaada wangu 2 siku zako zitakuwa nyingi, 2 na miaka itaongezwa katika maisha yako. 1
12Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; 2 kama wewe ni mtu wa mzaha, 2 wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” 1
13Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; 2 hana adabu na hana maarifa. 1
14Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, 2 juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji, 1
15akiita wale wapitao karibu, 2 waendao moja kwa moja kwenye njia yao. 1
16Anawaambia wale wasio na akili, 2 “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!” 1
17“Maji yaliyoibiwa ni matamu; 2 chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!” 1
18Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, 2 kwamba wageni wake huyo mwanamke 2 wako katika vilindi vya kuzimu.