Proverbs 7
1Mwanangu, shika maneno yangu 2 na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. 1
2Shika amri zangu nawe utaishi; 2 linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. 1
3Yafunge katika vidole vyako; 2 yaandike katika kibao cha moyo wako. 1
4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” 2 uite ufahamu jamaa yako; 1
5watakuepusha na mwanamke mzinzi, 2 kutokana na mwanamke mpotovu 2 na maneno yake ya kubembeleza. 1
6Kwenye dirisha la nyumba yangu 2 nilitazama nje kupitia upenyo 2 kwenye mwimo wa dirisha. 1
7Niliona miongoni mwa wajinga, 2 nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, 2 kijana asiye na akili. 1
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, 2 akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke 1
9wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, 2 giza la usiku lilipokuwa likiingia. 1
10Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, 2 hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu. 1
11(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, 2 miguu yake haitulii nyumbani; 1
12mara kwenye barabara za mji, 2 mara kwenye viwanja vikubwa, 2 kwenye kila pembe huvizia.) 1
13Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, 2 na kwa uso usio na haya akamwambia: 1
14“Nina sadaka za amani nyumbani; 2 leo nimetimiza nadhiri zangu. 1
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; 2 nimekutafuta na nimekupata! 1
16Nimetandika kitanda changu 2 kwa kitani za rangi kutoka Misri. 1
17Nimetia manukato kitanda changu 2 kwa manemane, udi na mdalasini. 1
18Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; 2 tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi! 1
19Mume wangu hayupo nyumbani; 2 amekwenda safari ya mbali. 1
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha 2 na hatakuwepo nyumbani karibuni.” 1
21Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; 2 alimshawishi kwa maneno yake laini. 1
22Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke 2 kama fahali aendaye machinjoni, 2 kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi, 1
23mpaka mshale umchome ini lake, 2 kama ndege anayenaswa kwenye mtego, 2 bila kujua itamgharimu maisha yake. 1
24Sasa basi wanangu, nisikilizeni; 2 sikilizeni kwa makini nisemalo. 1
25Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, 2 wala usitangetange katika mapito yake. 1
26Aliowaangusha ni wengi; 2 aliowachinja ni kundi kubwa. 1
27Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, + 7:27 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 2 ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.