Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 3

1Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, 2 bali zitunze amri zangu moyoni mwako, 1

2kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako 2 na kukuletea mafanikio. 1

3Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; 2 vifunge shingoni mwako, 2 viandike katika ubao wa moyo wako. 1

4Ndipo utapata kibali na jina zuri 2 mbele za Mungu na mwanadamu. 1

5Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote 2 wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 1

6katika njia zako zote mkiri yeye, 2 naye atayanyoosha mapito yako. 1

7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; 2 mche Bwana ukajiepushe na uovu. 1

8Hii itakuletea afya mwilini mwako, 2 na mafuta kwenye mifupa yako. 1

9Mheshimu Bwana kwa mali zako na 2 kwa malimbuko ya mazao yako yote; 1

10ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, 2 viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya. 1

11Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana 2 na usichukie kukaripiwa naye, 1

12kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, 2 kama vile baba afanyavyo 2 kwa mwana apendezwaye naye. 1

13Heri mtu yule aonaye hekima, 2 mtu yule apataye ufahamu, 1

14kwa maana hekima ana faida kuliko fedha 2 na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. 1

15Hekima ana thamani kuliko marijani; 2 hakuna chochote unachokitamani 2 kinachoweza kulinganishwa naye. 1

16Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; 2 katika mkono wake wa kushoto 2 kuna utajiri na heshima. 1

17Njia zake zinapendeza, 2 mapito yake yote ni amani. 1

18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; 2 wale wamshikao watabarikiwa. 1

19Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia, 2 kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; 1

20kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, 2 nayo mawingu yanadondosha umande. 1

21Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, 2 usiache vitoke machoni pako; 1

22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako 2 na pambo la neema shingoni mwako. 1

23Kisha utaenda katika njia yako salama, 2 wala mguu wako hautajikwaa; 1

24ulalapo, hautaogopa; 2 ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. 1

25Usiogope maafa ya ghafula 2 au maangamizi yanayowapata waovu, 1

26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako 2 na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego. 1

27Usizuie wema kwa wale wanaostahili 2 ikiwa katika uwezo wako kutenda. 1

28Usimwambie jirani yako, 2 “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: 2 wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. 1

29Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, 2 ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. 1

30Usimshtaki mtu bila sababu, 2 wakati hajakutenda dhara lolote. 1

31Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri 2 wala kuchagua njia yake iwayo yote, 1

32kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu, 2 lakini siri yake iko kwa mwenye haki. 1

33Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu, 2 lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. 1

34Huwadhihaki wale wanaodhihaki, 2 lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. 1

35Wenye hekima hurithi heshima, 2 bali huwaaibisha wapumbavu.

← Proverbs 2Read In The App, Free →Proverbs 4 →

Study Proverbs 3

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031