Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 11

1Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, 2 bali vipimo sahihi ni furaha yake. 1

2Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, 2 bali unyenyekevu huja na hekima. 1

3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, 2 bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao. 1

4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, 2 bali haki huokoa kutoka mautini. 1

5Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, 2 bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. 1

6Haki ya wanyofu huwaokoa, 2 bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya. 1

7Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; 2 yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu. 1

8Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, 2 naye mtu mwovu huingia humo badala yake. 1

9Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu 2 humwangamiza jirani yake, 2 bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa. 1

10Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; 2 mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha. 1

11Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, 2 bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa. 1

12Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, 2 bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake. 1

13Masengenyo husaliti tumaini, 2 bali mtu mwaminifu hutunza siri. 1

14Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, 2 bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika. 1

15Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, 2 bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama. 1

16Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, 2 bali wanaume wakorofi hupata mali tu. 1

17Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, 2 bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe. 1

18Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, 2 bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika. 1

19Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, 2 bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake. 1

20Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, 2 bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama. 1

21Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, 2 bali wenye haki watakuwa huru. 1

22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe 2 ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara. 1

23Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, 2 bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu. 1

24Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, 2 mwingine huzuia, lakini huwa maskini. 1

25Mtu mkarimu atastawi; 2 yeye awaburudishaye wengine 2 ataburudishwa mwenyewe. 1

26Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, 2 bali baraka itamkalia kichwani kama taji 2 yeye aliye radhi kuiuza. 1

27Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, 2 bali ubaya huja kwake yeye autafutaye. 1

28Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, 2 bali mwenye haki atastawi kama jani bichi. 1

29Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, 2 naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima. 1

30Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, 2 naye mwenye hekima huvuta roho za watu. 1

31Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, 2 si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?

← Proverbs 10Read In The App, Free →Proverbs 12 →

Study Proverbs 11

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031