Proverbs · Biblia (Kiswahili)

Proverbs 16

1Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, 2 bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana. 1

2Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, 2 bali makusudi hupimwa na Bwana. 1

3Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, 2 nayo mipango yako itafanikiwa. 1

4Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; 2 hata waovu kwa siku ya maangamizi. 1

5Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. 2 Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. 1

6Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; 2 kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya. 1

7Njia za mtu zinapompendeza Bwana, 2 huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. 1

8Afadhali kitu kidogo pamoja na haki 2 kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. 1

9Moyo wa mtu huifikiri njia yake, 2 bali Bwana huelekeza hatua zake. 1

10Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, 2 wala kinywa chake hakipotoshi haki. 1

11Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; 2 mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye. 1

12Wafalme huchukia sana kutenda maovu, 2 kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki. 1

13Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu; 2 humthamini mtu asemaye kweli. 1

14Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, 2 bali mtu mwenye hekima ataituliza. 1

15Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai; 2 upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli. 1

16Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, 2 kuchagua ufahamu kuliko fedha! 1

17Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; 2 yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake. 1

18Kiburi hutangulia maangamizi, 2 roho ya majivuno hutangulia maanguko. 1

19Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho 2 miongoni mwa walioonewa 2 kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi. 1

20Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, 2 tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana. 1

21Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, 2 na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho. 1

22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, 2 bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu. 1

23Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, 2 na midomo yake huchochea mafundisho. 1

24Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, 2 ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. 1

25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, 2 bali mwisho wake huelekeza mautini. 1

26Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; 2 njaa yake humsukuma aendelee. 1

27Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, 2 maneno yake ni kama moto uunguzao. 1

28Mtu mpotovu huchochea ugomvi, 2 nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu. 1

29Mtu mkali humvuta jirani yake 2 na kumwongoza katika mapito yale mabaya. 1

30Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; 2 naye akazaye midomo yake amenuia mabaya. 1

31Mvi ni taji ya utukufu; 2 hupatikana kwa maisha ya uadilifu. 1

32Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, 2 mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji. 1

33Kura hupigwa kwa siri, 2 lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

← Proverbs 15Read In The App, Free →Proverbs 17 →

Study Proverbs 16

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031